- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAHAKAMA YAMTANGAZA TSHISEKEDI MSHINDI WA UCHAGUZI
Mahakama ya kikatiba ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Alfajiri ya leo Jumapili January 20 imemtangaza Felix Tshisekedi kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais na kutupilia mbali madai ya Fayulu kwamba uchaguzi huo ulikuwa na udanganyifu.
Uamuzi huo wa kuthibitisha kuwa Tshisekedi ndiye aliibuka mshindi wa kinyang'anyiro hicho cha urais unakuja baada ya mahakama kupinga kesi iliyowasilishwa na kiongozi wa muungano wa upinzani wa LAMUKA Martin Fayulu, licha ya kuwa na mashaka makubwa ya kuwepo udanganyifu wa kura.
Fayulu anadai kwamba Tshisekedi na Rais Joseph Kabila walifanya mpango wa kisiri siri baada ya matokeo ya awali kuonesha kwamba mgombea ambaye alikuwa akiungwa mkono na Kabila, Emmanuel Ramazani Shadary, ameshika nafasi ya tatu katika uchaguzi huo.
Uamuzi huo wa mahakama unamaanisha kuwa sasa Tshisekedi anaweza kuapishwa kuwa rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ifikapo Jumanne wiki ijayo.
Fayulu ameitaka jumuiya ya kimataifa kupinga ushindi huo wa Tshisekedi kwa kutotambua mamlaka yake aliyoyataja yasiyoungwa mkono na Wacongo. Fayulu amejitangaza kuwa Rais halali wa Congo.