Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 9:44 am

NEWS: MAHAKAMA YAMSOMEA MASHTAKA HOSPITALINI MTUHUMIWA UBAKAJI

MARA: Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Mara imelazimika kuhamisha ofisi yake katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara mjini Musoma,kwa ajili maalum ya kumsomea shitaka la ubakaji mkazi mmoja wa kijiji cha Butiama anayedaiwa kukatwa ulimi wake kwa meno wakati wa tukio hilo la ubakaji.

Akisomewa shitaka hilo la ubakaji akiwa katika wodini katika hospitali ya rufaa mkoa wa Mara,mbele ya Hakimu mkazi Mfawidhi wa mahakama ya mkoa wa huo Mh Rahim Mushi,

mwendesha mashitaka wa serikali Frank Nchanila,amesema mtuhumiwa huyo Mathias Magembe Nyambereka mwenye umri wa miaka 23 anadaiwa kutenda kosa la Ubakaji Januari 6 majira ya saa sita na nusu usiku.

Amesema mtuhumiwa huyo akijifanya ni mwendesha bodaboda, walikula njama na wenzake wawili kisha kumbeba binti huyo na baada ya kuka vichakani na kutenda tukio hilo ndio mtuhumiwa akang’atwa ulimi na binti huyo wakati mtuhumiwa anapeleka mdomo wake kwa binti kwa ajili ya kumfanyia romansi.