- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAHAKAMA YAKUBALI KUFUTWA KAZI MLINZI ALIYEMPANGISHA WAZIRI FOLENI KENYA
Mahakama nchini Kenya imehalalisha hatua ya Mamlaka ya Uwanja wa Ndege Kenya kumfuta kazi aliyekuwa mlinzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Daizy Cherogony kutokana na Mlinzi huyo kumtaka aliyekuwa Waziri wa Elimu, nchini Kenya Fred Matiangi kukaa kwenye foleni akaguliwe.
Cherogory alifungua kesi mara tu baada ya kufukuzwa kazi mwaka 2007.
Cherogony alikataa kumruhusu Waziri Matiangi na timu yake ya usalama kuingia uwanja huo wa ndege bila kupitia sehemu ya ukaguzi
mfanyakazi huyo alikuwa anaitaka KAA kumlipa KSh2.4 milioni kama fidia
Afisa wa ulinzi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta ambaye alifutwa kazi kwa kutomheshimu Waziri Fred Matiang’i amepata pigo baada ya kesi yake kutupilia mbali.
Jaji Nzioki wa Makau alipuzilia mbali kesi ya Daizy Cherogony, kwa kushikilia kwamba namna mlalamishi alimkabili Matiang’i, ambaye kwa wakati huo alikuwa Waziri wa Elimu, ilikuwa sababu tosha kwa Mamlaka ya Safari za Ndege Nchini (KAA) kuchukua hatua za kinidhamu dhidi yake.
Jaji Nzioka alisema haki za mlalamishi katika kipengee cha 41 ya katiba zililindwa na utovu wake wa nidhamu ndio ulichangia kwake kupigwa kalamu.
“Alisikizwa kupitia sehemu ya 41 na haki zake chini ya kipengee cha 41(1) zililindwa.Kwa sababu kufutwa kwake kulitokana na utovu wa nidhamu, kesi hii imefutwa," alisema jaji huyo.