Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 9:42 pm

NEWS: MAHAKAMA YAKUBALI JOSHUA NASSAR KUVULIWA UBUNGE

Dodoma: Mahakama Kuu kanda ya Dodoma mbele ya Jaji Latifa Mansour, imekubali uamuzi wa Spika wa Bunge, Job Ndugai kumvua ubunge aliyekuwa Mbunge wa Alumeru Mashariki Joshua Nassari kwa Kile kinachoelezwa kuwa Mbunge huyo alishindwa kuhudhuria MIKUTANO mitatu ya Bunge mfululizo.

Machi 14, 2019 Ndugai alitangaza kumvua ubunge Nassari kwa kuiandikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) barua akiieleza kuwa Nassari amepoteza sifa ya kuwa mbunge baada ya kutohudhuria mikutano mitatu mfululizo bila kutoa taarifa.

Leo katika hukumu hiyo Jaji Mansour ametumia dakika 44 kusoma maelezo ya hukumu ya Mbunge huyo kijana.

Spika Ndugai aliitaja mikutano hiyo kuwa ni wa 12 ulioanza Septemba 4 hadi 14; Novemba 6 hadi 16, 2018 na wa Januari 29 hadi 9. Baada ya uamuzi huo, mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema amemuagiza Nassari kuzungumza na wananchi na wanachama wa jimbo lake kuwaeleza kilichotokea. Akisoma uamuzi wake leo Ijumaa Machi 29, 2019 Jaji huyo ametumia kifungu cha 5 (4) kuwa Nassari alipaswa kupeleka malalamiko yake kwa Katibu wa bunge wala si kama alivyofanya.

Kifungu kingine kilichombana Nassari ni cha kanuni ya 146 (2) kwamba alijifukuzisha mwenyewe kwa kutohudhuria vikao vitatu mfululizo vya Bunge bila taarifa. Mawakili wa Serikali, Alesia Mbuya, Masunga Kamuhanda na Pius Mboya walipangua hoja za wakili wa utetezi, Fred Kalonga aliyekuwa akipinga kuwa mbunge huyo alifukuzwa bila utaratibu hivyo kuitaka Tume ya Uchaguzi (NEC) isitangaze jimbo kuwa wazi.