- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAHAKAMA YAIFUTA BODI YA WADHAMAINI YA PROF. LIPUMBA
Dar es salaam: Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ambayo ipo karibu mita 100 kutoka Mahakama ya Rufaa imetengua uteuzi wa wajumbe wa bodi ya wadhamini wa Chama cha Wananchi (CUF) wa kambi ya Mwenyekiti anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba.
Uamuzi huo umetolewa leo Jumatatu Februari 18, 2019 na Jaji Dk Benhajj Masoud baada ya kubatilisha uteuzi wao.
Hata hivyo Jaji Masoud amesema majina yaliyokuwa yamependekezwa na kambi ya Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad hawakuwa na sifa ya kuteuliwa kuwa wajumbe wa bodi hiyo kwa kuwa nao hakuwa wamekidhi matakwa ya sheria.
Kesi hiyo ilifunguliwa na Mbunge wa Malindi (CUF) Ally Saleh alifungua kesi hiyo akipinga uamuzi wa Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi (Rita) wa kuwaidhinisha wajumbe waliopendekezwa na kambi ya Profesa Lipumba kuwa wajumbe wapya wa bodi hiyo
Kwa maana hiyo wajumbe wa bodi hiyo waliokuwepo awali wataendelea mpaka pale watakapoteua wajumbe wapya licha ya muda wao kupita.