- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAHAKAMA NCHINI KENYA YARUHURU TUME YA UCHAGUZI KUCHUGUZWA DATA
Nairobi: Mahakama ya Juu nchini kenya imeuruhusu muungano wa upinzani nchini humo (Nasa) kupekua saver zilizotumiwa na tume ya uchaguzi nchini humo wakati wa uchaguzi uliofanyika Agosti 8 mwaka huu.
Mahakama hiyo imesema kuwa muungano NASA utaweza kusoma data kwenye saver hizo chini ya uangalizi kuhakikisha usalama wa mitambo ya IEBC haidukuliwi
Kesi hiyo kimsingi imekuja baada ya Mgombea wa Nasa Raila Odinga kuwasilisha kesi mahakamani kupinga ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee mwaka huu.
Pia upinzani utapata utambulisho wa saver zilizotumiwa wakati wa uchaguzi, ukuta wa kinga uliotumiwa kulinda saver hizo pamoja na mitambo ya dijitali ya uchaguzi wa Kenya (KIEMS) dhidi ya wadukuzi na mfumo endeshi wa mitambo hiyo pamoja na nywila zilizotumiwa kuingia katika mitambo hiyo.
NASA wataruhusiwa kusoma nakala za Fomu 34A na 34B (fomu za matokeo katika vituo vya kupigia kura na ngazi ya maeneo bunge) ambazo zilitumiwa kutangaza matokeo.
Taarifa kuhusu mchakato wa upinzani kupekua sava na mitambo hiyo ya IEBC itawasilishwa kwa mahakama hiyo kesho jioni