Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 5:19 am

NEWS: MAHAKAMA KUU YA KENYA YATIA HOFU JUU YA KESI YA UCHAGUZI

Nairobi: Mahakama ya juu nchini Kenya, leo Jumatano imewatahadharisha wadau wa kesi iliyowasilishwa kwake kuhusu uchaguzi wa urais dhidi ya kuizungumzia hadharani hadi pale litakaposhughulikiwa tarehe mosi mwezi Septemba.

Taasisi hiyo ya juu nchini kenya imewataka waliokuwa wagombea urais, wafuasi wao, mawakala, na tume ya uchaguzi na mipaka, kusita kuzungumzia kesi hiyo nje ya mahakama.


Tangu muungano wa NASA kuwasilisha hoja yao mahakamani kufuatia kutangazwa kwa rais Uhuru Kenyatta kama mshindi wa uchaguzi huo wa tarehe 8 mwezi huu, viongozi wa kisiasa wa mrengo huo na hata wale wa mrengo wa Jubilee, wamekuwa wakitoa kauli kuhusu kesi hiyo katika mikutano ya hadhara.