- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAHAKAMA KUAMUA DHAMANA YA MWANAHABARI SEBASTIAN ATILO
IRINGA: Jana ilikua ni siku ya kusikiliza mapingamizi yaliyowekwa na wakili wa THDC Emmanuel Chengula anaemtetea Mwandishi wa habari Sebastian Atilio anayekabiliwa kwa makosa mawili yaani kutoa taarifa ya uongo na kufanya kazi ya uandishi bila kuthibitishwa na bodi.
mapingamizi hayo ni dhidi ya maombi yaliyopelekwa na jamhuri kumzuia mwandishi huyo kutopewa dhamana kwa hofu ya usalama wake dhidi ya RAIA wa kijiji cha ifupira.
Pamoja na hayo mahakama ya wilaya ya Mufindi mbele ya Hakimu Mkazi Edward Uforo ilisikiliza mapingamizi yote manne na kuahirisha kesi hiyo mpaka tarehe 25/09/2019 ambapo itatoa maamuzi juu ya hatima ya dhamana ya mwandishi Huyo wa habari.
Hata hivyo kesi yake ya msingi itatajwa tarehe 25/09/2019 Mara baada ya kusomwa kwa uamuzi unaotokana na mapingamizi yaliyo wekwa.