Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 2:42 am

NEWS: MAHAKAMA KENYA IMESHINDWA KUTOA UWAMUZI MAPENZI YA JINSIA MMOJA

Mahakama kuu nchini Kenya leo Ijumaa Feb 22 imeahirisha kutoa uamuzi kuhusu uhalali wa sheria inayoharamisha mapenzi kwa watu wanao jihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Uamuzi uliopangiwa kutolewa hii leo ulikuwa umetarajiwa sana sio nchini Kenya tu, bali pia katika bara zima la Afrika.

Kwa upande wa Jaji katika mahakama hiyo hii leo asubuhi, amesema kesi hiyo imelazimika kuhairisha kutokana na kuzidi kwa majukumu katika mahakama hiyo.

Sheria za Kenya, zinatamka wazi kuwa mapenzi ya jinsia moja ni hatia iliyo na hukumu ya miaka 14 gerezani, sheria hiyo na sawa na sheria zilizopo kwenye mataifa mengi barani Afrika

Brian na Yvonne ni watetezi wa haki za jamii ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja, pamoja na wale waliojibadilisha jinsia na hisia na pia ni washiriki katika mapenzi hayo

''Tunadharuliwa, tunakabiliwa na ghasia, tunaumia, tunateswa, tunakosewa. Tukienda kutafuta huduma za afya tunaangaliwa kwa dharau, tunatukanwa, tunatemewa mate, tunafanywa kama sisi sio Wakenya, na kama sisi sio Binaadamu, ni kama sisi ni viumbe wasiotoka katika dunia hii'.

Brian na Yvonne ni wanaharakati wa kutetea haki za jamii ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja

''Unapata, wakati mwingi mtu akisema kitu kibaya au kufanya kitu kibaya dhidi ya jamii yetu. Mtu anasema, hata Kenya hairuhusiwi, sheria inapinga, kwa sababu sio watu wengi wanaokwenda kwenye hicho kifungu cha sheria kuelewa inasema nini. Yeye amesikia tu sheria, inasema,' amefafanua Yvonne.