- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAHAKAMA IRINGA IMEYATUPILIA MBALI MAOMBI YA KUMUONDOA MEYA
Mahakama ya mkoa wa Iringa imetupilia mbali maombi ya kuzuia mchakato wa kumuondoa madarakani Meya wa Manispaa ya Iringa Alex Kimbe kupitia chama cha Chadema.
Akitoa maamuzi hayo leo Machi 27, 2020 Hakimu mkazi wa Mahakama ya mkoa wa Iringa Aden Kanje amesema maombi yaliyowasilioshwa yalikosewa na hivyo kuifanya mahakama hiyo kushindwa kuisikiliza kesi hiyo kwa mujibu wa sheria.
Awali kikao cha kuendesha mchakato wa kumng’oa Meya Kimbe jana tarehe 26 Machi 2020, kilikwama baada ya madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutohudhuria. Hata hivyo, Hamid Njovu, Mkurugenzi wa Halmshauri ya Manispaa ya Iringa, ameitisha Mkutano Maalumu wa Baraza la Madiwani la manispaa hiyo, kesho tarehe 28 Machi 2020. Miongoni mwa ajenda ya kikao hicho kesho, ni kupiga kura ya kutokuwa na imani na Meya Kimbe.
Meya Kimbe (Chadema), alianza kusakamwa na baadaye kupewa barua ya kujieleza kutokana na kupewa tuhuma nne.
Tuhuma hizo ni ukosefu wa adabu, matumizi mabaya ya madaraka, matumizi mabaya ya rasilimali za halmashauri na vitendo vya rushwa. Tarehe 2 Machi 2020, Meya Kimbe alisema amepokea barua iliyobeba tuhuma hizo za kupikwa kwa sababu maalum za kisiasa.
“Nitapeleka barua kwa mkurugenzi wa manispaa ili nimweleze na kumkumbusha vyombo vya usalama na watendaji wake taratibu na kanuni za kumtoa Meya madarakani wamezikosea,” alisema. Meya Kimbe alisema, CCM, kimekosa fursa kwa wananchi na sasa kinatumia hila kukabili maeneo yanayoongozwa na wapinzani ikiwemo Manispaa ya Iringa.