Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 9:36 am

NEWS: MAHAKAMA CONGO YATOA WARANTI KUKAMATWA KIONGOZI WA KIVITA

Mahakama ya kijeshi ya mkoa wa Kivu Kaskazini imetoa waranti wa kukamatwa dhidi ya kiongozi wa kivita Guidon Shimiray Mwissa, anaye shtumiwa kutekeleza uhalifu mbalimbali katika eneo hilo.

Related image

"Guidon Shiniray Mwissa anakabiliwa na mashitaka ya kushiriki katika kundi la waasi", "uhalifu wa kivita kwa kuwasajili watoto katika kundi lake" na "uhalifu dhidi ya ubinadamu kwa ubakaji". Haya ni mashitaka yaliyomo kwenye waranti huo uliotolewa dhidi ya Guidon Shimiray Mwissa na mahakama ya kijeshi, ambayo ilifunguliwa kesi dhidi yake mnamo mwezi Machi 2018. Tangu wakati huo, waathirika kadhaa wamesikilizwa, amesema Mwendesha mashitaka wa kijeshi, Jenerali Timothy Mukuntu.

Related image

Guidon Shiniray Mwissa ambaye Tayari anakabiliwa na vikwazo vya Umoja wa Mataifa, anaongoza muungano wa makundi ya waasi wa NDC-R (Nduma Defense of Congo-Renove) tangu mwaka 2015. Kundi ambalo linaendesha vita dhidi ya makundi ya wapiganaji wa Kihutu kutoka nje na yale yanayoundwa na baadhi ya raia wa DRC katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

Katika miezi ya hivi karibuni, kwa mujibu wa vyanzo vya Umoja wa Mataifa, Guidon Shimiray Mwissa alipanua eneo lake la kivita kwa kiasi kikubwa, na hatimaye kudhibiti "miji na maeneo ya uchimbaji madini ya Walikale," lakini pia maeneo ya Lubero, Masisi na Rutshuru.