Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 11:03 pm

NEWS: MAGUFULI "MAKAMPUNI YA SIM YASIYO JISAJILI SOKO LA HISA(DSE) YAFUTENI MSIPIGE FINE"

Dar es salaam: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Mafufuli leo amewataka wamiliki wote wa mitandao ya mawasiliano kujisajili kwenye soko la hisa la Dar es salaam (DSE) ili iwe rahisi kutozwa kodi halisi wanayo takiwa kuliapa, Rais Magufuli ameyataka makampuni kama Vodacom, Tigo, AirTel, na zantel kujisajili akasema kuwa kuto kufanya hivyo ni kuikosesha serekali kupata kipato na ninjia ya kukwepa kulipa kodi halisi.

Akiongea kwenye hafla ya kuzindua Data Center ya kulipa KODI iliyopo kijitonyama jijini Dar es salaam, kuwa yapo makampuni ya simu yanayo kwepa kulipa Kodi kwa sababu ya kuto kujisajili kwenye soko la hisa la Dar es salaam, Rais akaagiza mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA Kuyafutia usajili makampuni yote yatakayo kataa kuingia kwenye soko hilo la hisa,"Tulipitisha sheria kwa makampuni ya simu yote yawe registered kwenye Dar es salaam stock of exchange DSE, yamesua sua weee, yamezunguka weee, yamefanya weee angalau Vodacom wamejitahidi jitahidi wengine bado"

Aliongeza kuwa " TCRA imekuwa ikiyatoza faini makampuni ya mtandao ya mawasiliano kwa kukosa kujisajili au kukwepa kodi, faini yenyewe sijui milioni 300 ni ndogo ukilinganisha na faida wanayo pata, kwa mtu anaye pata mabilioni ataacha kujirejista kwenye DSE Kusudi uwe unampiga fine, kwa sababu faidi nyingi anabaki nayo ni bora makampuni yote ambayo hayataki kuingia kwenye soko la hisa la Dar es salaam yafuteni kabisa lazima tufike mahali tutoe decision hata kama zinauma " Aliongea Rais Magufuli

Pia Rais Magufuli alizungumzia viwanda kuwa tuliwahi kubinafsisha 1992 lakini zaidi ya viwanda 197 vilikufa kwa kushindwa kuendelezwa

Pia hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa serekali akiwemo Makamu wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassani, Rais wa Baraza la mapinduzi wa Zanziba Dr. Ali Mohamed shein, Waziri wa Ujenzi Makame Mbarawa, Waziri wa fedha Dr. Philipo Mpango na viongozi wengine,