Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 2:10 am

NEWS: MAGUFULI AVITAKA VYOMBO HUSIKA WAKAWAHOJI WAKINA CHENGE

Dar es salaam: Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mh. Dr. John pombe Magufuli leo tarehe 12 juni 2017 amekabidhiwa ripoti ya kamati ya pili ya kuchunguza madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga wa madini, amabayo yaliyokusanywa kutoka maeneo mabali mbali hapa nchini. Kamati hiyo inaongozwa na Mwenyekiti wake, Profesa Nehemiah Osolo, imewasilisha ripoti hiyo ikiwa ni siku 18 baada ya kamati ya kwanza kuwasilisha ripoti yake.

Rais alizungumza mengi baada ya kukabidhiwa ripoti miongoni mwa hayo ni kauli ya kusema kuwa hata shetani huko alipo atakuwa anawacheka Watanzania kutokana na umaskini wa kujitakia.
Amesema Mungu amelibariki taifa kuwa na kila aina ya madini lakini umaskini umeendelea kuwatafuna Watanzania.
Amesema Mungu alitupenda Watanzania, akatuweka katika nchi ya Tanzania, lakini kwa upendo mkubwa, akatuwekea maliasili nyingi, ili ziwalishe Watanzania.


“Ukiangalia madini tuliyonayo ni ya kila aina, si machache, tuna copper, silver…madini yote yako Tanzania , tumepewa hadi hellion, inayopatikana katika nchi tatu tu duniani, lakini pamoja na madini hayo yote, hadi Tanzanite inapatikana Tanzania tu, lakini pamoja na mali hiyo yote Mungu kutupendelea, Watanzania tumebakia maskini nina uhakika hata shetani huko aliko anatucheka kwa kuwa umaskini wetu ni wa kujitakia,"amesema.

Rais Magufuli amesema lakini inawezekana shetani huyo huyo aliwatumia baadhi ya viongozi wa taifa hili kulifanya maskini.Ameongeza; “lakini shetani huyo huyo bado hajachoka amekuwa akiwatumia Watanzania baadhi kupinga juhudi tunazozifanya katika kulikomboa taifa.”
"Waheshimiwa mara baada ya kupokea ripoti kama hii, inayotia uchungu sana nina uhakika kwa Mtanzania yeyote mwenye akili timamu ukisikia ripoti kama hii itakutia uchungu sana, ndiyo maana nashindwa nianzie wapi, nashindwa nizungumze nini lakini nisije kusahau ninawapongeza kamati, mliofanya kazi kwa niaba ya Watanzania.


"Nafahamu wapo wengine walitaka hata kuhatarisha maisha yenu, mlitanguliza maslahi ya Taifa, Watanzania wanaopenda mali yao itumike kwa maslahi yao wataendelea kuwaombea,"amesema.