Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 2:45 pm

NEWS: MAGEREZA 14 MOROGORO ZIMEKATIWA UMEME ZIPO GIZANI MWEZI SASA

DODOMA: MBUNGE wa Viti Maalum , Devotha Minja (Chadema) amesema kauli ya hivi karibuni ya Rais John Magufuli kuagiza Shirika la umeme nchini (TANESCO) kukata umeme imesababisha magereza 14 katika mkoa wa Morogoro kukatiwa umeme na kusababisha wafungwa kuishi katika giza tororo.

Kutokana na kukatiwa umeme kwa magereza hizo askari wanalazimika kutumia tochi,vibatali katika nyumba zao kutokana na wao pia kukatiwa umeme jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa askari magereza na wafungwa pia.

Devotha ametoa kauli hiyo jana bungeni wakati akiuliza swali la nyongeza kwa kutaka kuelewa kama kitendo cha magereza 14 katika mkoa wa morogoro kukatiwa umeme kwa kutekeleza agizo la Rais la (KA-TA) kama siyo ukiukwaji wa haki za mfungwa ambazo serikali ya tanzania ulisaini katika mkataba wa Umoja wa mataifa.

Devotha amesema kutokana na kauli ya rais ya kuelekeza TANESCO kukata umeme katika taasisi mbalimbali sasa ni takribani mwezi mmoja katika magereza 14 za morogoro hazina umeme pamoja na nyumba za askari jambo ambalo linasababisha wafungwa hao kunyimwa haki zao za kuishi katika sehemu yenye mwanga wa kutosha.

Pia alisema maaskari magereza wanalazimika kutumia vibatali jambo ambalo ni hatari katika kulinda usalama wao pamoja na usalama wa wafungwa hao ambao kimsingi wanatakiwa kupata hiki yao ya kuishi katika eneo ambali linaendana na mikataba ya haki ya mfuungwa ya umoja wa mataifa.

Akiendelea kuuliza maswali ya Nyongeza Devotha alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kukarabati magereza au kujenga magereza mapya au kuyapanua ili kuondokana na usumbufu mkubwa ambao wafungwa wanaupata kutokana na kuwepo kwa msongamano mkubwa gerezani.


Awali katika jimbi la msingi la mbunge wa Viti Maalum,Zubeda Sakuru (Chadema) alitaka kujua serikali ina mkakati gani katika kufanya matengenezo na kulinda haki za wafungwa.

“Maagereza mengi nchini hayo katika Viwangona ubora na hivyo kuvunja haki za wafungwa,Je serikali ina mkakati gani katika kufanya matengenezo na kulinda haki za wafungwa” amehoji Zubeda.

Akijibu maswali hayo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwiguru Nchemba, alikiri kuwa magereza hizo hazima umeme kutokana na kauli ya KA-TA lakini suala hilo kwa sasa linashughulikiwa na malipo na ankra ya umeme italipwa.

Amesema taasisi nyingi za serikali ikiwemo magerza zimekumbana na adha ya kukatiwa umeme lakini hiyo ni kutokana na kufanya wahusika wa malipo kuwa makini na kuheshimu fedha za serikali kwa kutumia katika matumizi ambayo yamekusudiwa.

Akizungumzia ujenzi na upanizi wa magereza Mwigulu alisema kwa sasa wanajenga magereza kubwa katika maeneo ya kilimo na magereza zilizopo mijini zitakuwa kwa ajili ya mahabusu kwa nia ya kupunguza safari ndefu pindi wanapokuwa wakipelekwa mahakamani.

Akijibu swali la msingi Mwigulu amesema Jeshi la magereza limekuwa katika kusimamia haki za wafungwa kwa kuzingatia sheria ya magereza No.34 ya Mwaka 1967 na kanuni za uendeshaji wa magereza za mwaka 1968.