- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAGAIDI WALIPUA HOTEL YA KITALII KENYA
Mlipuko mkubwa sambamba na milio ya risasi ilisikika Jumanne ya leo mchana katika hoteli moja Magharibi wa jiji kuu la Kenya Nairobi( Dusit hoteli ), katika shambulizi ambalo kundi la kigaidi la Al Shabab nchini Somalia linasema limehusika kwa asilimia 100.
Taarifa zinasema kuwa, watu kadhaa wamejeruhiwa lakini idadi haijatajwa katika tukio hilo lililotokea katika hoteli hiyo inayofahamika kama Dusit.
Aidha, haijafahamika iwapo kuna watu waliopoteza maisha katika tukio hili ambalo jeshi la polisi linasema ni la kigaidi.
“Leo mchana, karibu saa tisa hivi, watu wenye silaha walivamia eneo lililo na hoteli na ofisi na kufwatua risasi.Tunashuku ni tukio la kigaidi,” alisema Joseph Boinett Inspekta Mkuu wa jeshi la Polisi nchini humo.
“Maafisa wetu bado wanaendelea na operesheni ili kuwaondoa watu hao wenye silaha, lakini tayari tumewaokoa watu wengi sana,” aliongeza.
Wachambuzi wa masuala ya usalama, wanasema maafisa wa usalama wamejitahidi kushughulikia tukio hili kinyume na mambo yalivyokuwa wakati wa mashambulizi yaliyopita.
Shambulizi hili, limewakumbusha wengi shambulizi la kigaidi lilitokea mwaka 2013 katika jengo la biashara la Westgate na kusababisha vifo vya watu 67.
Mwezi Aprili mwaka 2015 shambulizi lingine la kigaidi lilitokea katika Chuo Kikuu cha Garissa Mashariki mwa nchi hiyo na kusababisha vifo vya watu 148, wengi wao wakiwa wanafunzi.
Kenya ilianza kushuhudia milipuko ya kigaidi kutoka kwa kundi la Al Shabab mwaka 2011, baada ya kuwatuma wanajeshi wake nchini Somalia, kupambana na kundi hilo la kigaidi ambalo linapambana na serikali ya Mogadishu.