Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 5:04 am

NEWS: MADIWANI WATAKIWA KUDUMISHA AMANI.

BAHI: Katika kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma wametakiwa kuanza kufanya maandalizi ya amani mapema na kuepuka kuzalisha migogoro isiyokuwa na tija lengo ikiwani ni kufanya uchaguzi wa amani na wahaki.



Hayo yameelezwa na Afisa Serikali za Mitaa Emmanuel Kuboja wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya nne ya mwaka wa fedha 2018/2019 kilichofanyika Wilayani hapo.



Akiwasilisha salama za Mkuu wa Mkoa Kuboja amesema kuwa sehemu yeyote yenye utulivu hata maendeleo yake huwa makubwa hivyo amewaagiza Madiwani kuundelea kuwa watulivu na kudumisha amani .



Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Danford Chisomi amesema kuwa Halmashauri itaendelea kutoa mchango wake katika kila sehemu ambapo itahitajika kufanya hivyo .ili kuendelea kukuza na kusimamia miradi mbalimbali .

Chisomi ameyasema hayo alipokuwa akijibu baadhi ya changamoto zilizoelezwa na baadhi ya Madiwani na hasa katika suala la ujenzi wa maboma na mdarasa katika kata mbalimbali

Hata hivyo Chisomi amesema kuwa ni lazima kuendelea kuungana ili kuongeza nguvu kwa ajili ya kuendelea kusimamia miradi mbalimbali iliyopo ndani ya Halmashauri.

Amewataka Madiwani kuendelea kushikamana ili kuhakikisha miradi yote iliyoanzishwa inaenda vizuri na inakamilika kulingana na thamani ya pesa iliyopangiwa.

Hata hivyo Chisomi ameseama kuwa Halmashauri imeanza kutoa zawadi kwa viongozi wanaosimamia kazi zao vizuri pamoja na kufanya kazi zao kwa weledi na kudai kuwa zoezi hilo limeshaanza kwa watendaji wa Kata na Vijiji ambao wameendelea kufanya vizuri, na amesema kuwa zoezi hili ni endelevu hata kwa wakuu wa idara mbalimbali pia


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Dk Fatuma Mganga amewaagiza Madiwani kuendelea kuwaelimisha wananchi kuendelea kutoa michango yao mbalimbali katika kuisaidia halmashauri kuboresha baadhi ya miradi.

Pia amewataka wakuu wa idara mbalimbali kushirikisha sekta binafsi pia na baadhi ya vikundi katika kushiriki kuendelea kusimamia miradi midogomidogo iliyopo ndani ya halmashauri