- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MADIWANI WA CHADEMA MBARONI KWA WIZI WA MILIONI 10
Songwe: Madiwani wawili wa Chadema wa Halmashauri ya Mji ya Tunduma wilaya ya Momba wanashikiliwa na polisi wakituhumiwa kwa makosa tofauti, Madiwani hao ni Emmanuel Mwalupasa na Jailo Mwandute wote wa wilaya hiyo.
Akiongea na Muakilishi Publisher kwa Njia ya simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Mathias Nyange amesema kuwa Diwani Mwalupasa ambaye ni diwani wa Mpande anatuhumiwa kufunga ofisi ya afisa mtendaji wa kata kata hiyo kwa siku tatu mfululizo bila sababu za msingi.
Naye Diwani wa Mwandute wa Kata ya Katete,Kamanda Matias amesema anatuhumiwa kwa wizi wa zaidi ya Sh10 milioni ambazo zilikuwa fedha za maendelo ya kata hiyoKamanda Nyange amesema madiwani hao walikamatwa jana Alhamisi jioni na kufikishwa kituo kikuu cha polisi mjini Tunduma ambako wanaendelea kushikiliwa.
Nyange amesema kuwa uchunguzi kuhusu tuhuma zinazowakabili madiwani hao unaendelea.