- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MADIWANI KIGOMA WAFUTA POSHO ZOTE ZA WENYEVITI WA MTAA 68
Baraza la Halmashauri ya Kigoma Ujiji linaloongozwa na chama cha Act Wazalendo limekubaliana kwa kauli moja na kupitisha azimio la kutokuwalipa posho wenyeviti wote wa Serikali za Mitaa wapatao 68 waliopita kupitia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Novemba 2019.
Chama hicho kimedai Wenyeviti hao walipita katika uchaguzi huo kibatili.
Hoja ya kutowalipa posho viongozi hao wa Serekali ya Mitaa iliibuliwa na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ili kuonesha kulaani kilichofanyika katika uchaguzi ule wa mwaka jana.
Katika Uchaguzi huo uliogubikwa na hila chuki, na Sintofahamu Jumla ya vyama vinane vilijitoa katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika , Novemba 24, ikiwa imebaki miezi michache kabla ya nchi hiyo kuingia kwenye Uchaguzi Mkuu.
Uchaguzi huo hufanyika chini ya Ibara ya 8 (1) (a) ya Katiba ya Tanzania kuwa ni nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki ya kijamii na kuwa ndiyo msingi wa mamlaka yote iliyonayo serikali hupata kutoka kwa wananchi.
Vyama vilivyotangaza kujitoa kushiriki kinyang'nyiro cha uchaguzi huo ni Chadema, UMD, CCK, NCCR-Mageuzi, NLD, ACT-Wazalendo, CUF na Chauma.
Uamuzi wao umetokana na malalamiko mbalimbali yaliyowasilishwa mbele ya umma na kukilaumu chama tawala CCM kuwa chanzo cha kuvurugika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu nchini.
Licha ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Seleman Jaffo, mwenye dhamana ya uchaguzi huo kutoa matamko mawili yenye nia ya kuviomba vyama vya upinzani kulegeza misimamo yao na kuwataka wagombea walioteuliwa kuendelea na uchaguzi huo, lakini hapakuwa na mafanikio yoyote.
Vyama vya kisisasa vyakosolewa
Katika taarifa yake iliyokaririwa na vyombo vya habari nchini, Waziri Jaffo alivikosoa pia vyama vya siasa kwa kile alichokiita kushindwa kuwalekeza wagombea wao namna nzuri ya kujaza fomu za kuomba kuteuliwa katka nafasi wanazogombea kwenye mitaa,vitongoji na na vijiji.
"Inaonesha vyama vya siasa vilishindwa kuwasimamia wagombea wao wakati wa kujaza fomu hizo, kwa maana makosa mengine yalionekana ni kama ya mtu alijaza ili kushindwa mapema." Hilo alilitoa wakati anazungumzia suala la vyama vya siasa kujitoa kwenye uchaguzi huo, lakini vyama vilivyojitoa vilisimama kidete na kupinga mchakato mzima wa uchaguzi.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akizungumza na vyombo vya habari mwanzoni mwa mwezi Novemba alibainisha kuwa chama chake kimeshuhudia wagombea wake wote katika Mkoa wa Mwanza wakielezwa kukosa sifa. Mbowe alisema takribani wagombea 1,000 walienguliwa na wasimamizi wa uchaguzi huo.