- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MADIWANI DAR WAMLAANI PROF. LIPUMBA
Dar es salaam: Madiwani 19 kati ya 21 wa Chama cha Wananchi (CUF), wanao liwakilisha jiji la Dar es Salaam, wameunga mkono msimamo wa Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad, kuhusiana na usajili wa bodi mpya ya udhamini wa chama hicho.
“Tunapinga juhudi zinazofanywa na Prof. Lipumba na wafuasi wake wote ambao wamekua na vitendo na mwenendo usiofaa, wa kuharibu mali za chama, kuiba fedha za ruzuku, kusababisha uvunjifu wa amani na kuharibu taswira ya chama mbele ya jamii,” amesema Musa Kafana.ambaye ni naibu meya na muakilishi wa madiwani hao.
Naibu meya huyo amelaani njama na mipango ya Jaji Francis Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kwa kumtambua na kuwataka wana CUF wamrudishe Lipumba katika nafasi ya uenyekiti kwa madai alitengua barua yake ya kujiuzulu.
“Si Jaji Mutungi wala Profesa Lipumba aliyeweza mpaka leo hii kuwaeleza wana CUF na watanzania kwa ujumla ni Ibara ipi ya katiba ya CUF inayoruhusu kiongozi akijiuzulu anayo haki ya kutengua kujiuzulu kwake kwa kumuandikia barua katibu wa mamlaka iliyomchagua,” amesema.
Kafana amesema madiwani wa CUF pia wanapinga na kulaani kitendo cha Mamlaka ya usajili wa vizazi na vifo – RITA kwa uamuzi wake wa kusajili majina ya wajumbe wapya wa bodi ya udhamini ya CUFkinyume na kifungu cha 26 cha sheria ya wadhamini (The Trustees’ Incorporation Act Cap. 318).
“Tunaungana na pendekezo la chama cha kuwakilisha maombi mbele ya mahakama kuu kuitaka isimamishe kesi nyingine zote zilizofunguliwa na chama kuhusiana na kadhia hii hadi hapo shauri linalohusu uhalali wa maamuzi ya Rita litakapoamuliwa.”
Aidha, madiwani hao wamelaani pia hatua ya Ally Happi, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kuamuru Halima Mdee, Mbunge wa Kawe awekwe rumande masaa 48 kwa tuhuma ya kumkashifu Rais John Magufuli.
“Halima Mdee ni sehemu ya madiwani katika jiji la Dar es Salaam, lakini pia ni Mjumbe wa baraza la jiji. Sisi chama cha Wananchi – CUF tunalaani kitendo hiki kwasababu tunaona ni ukiukwaji wa haki za binadamu maana kila mtu ana uhuru wa kujieleza na kutoa maoni yake,” amesisitiza Kafana.