Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 12:25 am

NEWS: MADEREVA WAZEMBE KUCHAPWA BAKOLA

DODOMA: SERIKALI imesema katika kupunguza ajali za majeruhi imeazimia kuja na mkakati namba mbili ambapo katika utekelezaji wake hatua zitakazo chukuliwa ni pamoja na madereva kuchukuliwa hatua kali za Kisheria ikiwemo kuwapiga viboko.

Kauli hiyo imetolewa leo Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi,HAMAD YUSUFU MASAUNI wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tathmini ya utejkelezaji wa mpango mkakati wa kupunguza ajali za barabarani katika kipindi cha miezi sita kuanzia Agosti2016 hadi Januari 2017.

MASAUNI amebainisha kuwa kutokana na tathmini ya mpango mkakati huo kufanikiwa katika eneo la kupunguzaajali za majeruhi kwa kuvuka lengo walilojiwekea la asilimia kumi na kufikia asilimia 13 huku ajali zilizosababishavifo zilipungua kwa asilimia 8 na hivyo wameamua kuja na mpango mkakati huo namba mbili.

Aidha amebainisha kuwa mpango huo utakuwa na usimamizi wa mfumo wa nukta katika leseni za udereva ambapo dereva akifanya kosaataunganishwa na mfumo wa Mamlaka ya mapato TRA na kunyanga’anywa leseni.