- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MACHIMBO YA DHAHABU NHOLI YAWATESA WANANCHI.
DODOMA: Baada ya Siku chache kupita wananchi wa kijiji cha Nholi wilayani Bahi mkoani Dodoma kuomba Rais Dkt John Magufuli kufungia machimbo ya dhahabu ya Nholi kwa madai hayawasaidii kimaendeleo,serikali wilayani Bahi imeagiza Takukuru kuwachunguza viongozi wa kijiji kwa tuhuma za ubadhilifu wa zaidi ya shilingi milioni 20 za wachimbaji wadogo walizotoa kwa ajili ya maendeleo ya kijiji.
Mapema hivi karibuni mtandao wa muakilishi uliripoti taarifa za wananchi wa kijiji cha Nholi wakitaka kufungwa kwa machimbo ya dhahabu yaliyopo kijijini hapo ambapo madai yao makubwa ni kwamba licha ya kuwepo kwa machimbo hayo ya dhahabu wamekuwa hawanufaiki na shughuli za kimaendeleo
Kufuatia tuhuma hizo Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Bahi Elizabeth Kitundu alifika katika machimbo hayo na kuagiza uchunguzi kufanyika kwa mali na fedha zilizotolewa na wachimbaji kwa ajili ya maendeleo ambazo zimekuwa haziwafikii wananchi.
Akizungumza kwa niaba ya wachimbaji wadogo katika machimbo hayo Mwenyekiti wa wachimbaji hao Nelly Mwamsuva alisema wachimbaji wamekuwa wakichangishwa tozo mbalimbali na viongozi wa kijiji ambapo walisema wanashangazwa na kitendo cha kuambiwa kuwa hawachangii shughuli za maendeleo
Akijibu tuhuma zinazoikabili serikali ya kijiji Mwenyekiti wa kijiji hicho Carolina Ezekiely amesema kuwa tuhuma zinazosemwa na wananchi juu ya ubadhilifu hazina ukweli na kwamba fedha zinazochangishwa zinakwenda kwenye shughuli za maendeleo
Silimu Mtigile ni Afisa madini mkoa wa Dodoma alisema mgodi huo unatambulika na unachangia pato la taifa huku akiitaka jamii katika eneo hilo kuwa na uhusiano mzuri ili kuepusha migogoro na wote wanufaike na rasilimali hiyo
Baadhi ya wananchi bado wanaendelea kulia na serikali wakiiomba kuhakikisha kijiji kinanufaika na rasilimali hiyo muhimu kwa maendeleo yao