Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 3:44 am

NEWS: MABOSS WAWILI WA VODACOM WAJIUZULU

Dar es Salaam. Wakurugenzi wawili wa bodi ya kampuni ya Mawasiliano nchini Tanzania Vodacom Tanzania, wametangaza kujiuzulu.

Wakurugenzi hao ni Andries Delport na Till Streichert ambao walikuwa wafanyakazi wa Vodacom Group ya Afrika Kusini.

Image result for vodacom ofisi tanzania

Tangazo lililotolewa na kampuni hiyo leo Jumatatu, Desemba 23, 2019 imesema Delport atajiuzulu Mei 14, 2020 wakati Sreichert akitarajiwa kujiuzulu Juni 30, 2020 au muda wowote kabla ya tarehe hiyo.

Ripoti ya hivi karibuni ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zinaonyesha kampuni hiyo inao zaidi ya wateja milioni 15 kati ya milioni 47 waliosajiliwa na mamlaka hiyo

Image result for Andries Delport and Till Streichert Till Streichert

Kabla ya kuingia Vodacom Novemba 2017, Till alikuwa mjumbe wa bodi ya kampuni ya Safaricom ya Kenya kuanzia Agosti 2017.

Wakati Till akiwa ofisa mkuu fedha wa kampuni hiyo kuanzia Februari 2014 Delport alikuwa mkuu wa kitengo cha teknolojia.

Akiwashukuru kwa mchango walioutoa kwa muda waliohudumu, katibu wa Vodacom Tanzania, Caroline Mduma amesema: “Bodi inawashukuru na kuwatakia mafanikio mema katika shughuli zao.” Wajumbe hao wametangaza kujiuzulu ikiwa ni miezi mitano tangu aliyekuwa mwenyekiti wao, marehemu Ali Mufuruki kufanya hivyo.

Mufuruki alitangaza nia hiyo Agosti akiijulisha kuachana nayo kuanzia Desemba Mosi, 2019 na wiki tatu baada ya utekelezaji huo, wajumbe hao wawili wametoa notisi ya miezi sita kuachana nayo.