- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAANDALIZI 88 YADODA
DODOMA: LICHA ya kutakiwa kuwepo kwa maandalizi mapema ya maoneshi ya wakulima Nanenane, lakini maoneshi hayo kanda ya kati yameonekana kudolola.
Hali ya mdololo imeoneshwa zaidi na halmashauri ya Chamwino,halmashauri ya Kongwa zote za mkoani Dodoma ,Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi pamoja na Halmashauri ya Singida ambapo jadi August 3 mwaka huu bado mabanda ya maonesho yalikuwa hayana maandalizi yoyote.
Baadhi ya washiriki ambao waliweza kuzungumza na MUAKILISHI walieleza kuwa ni bora kuyafuta maonesho ya Nane nane kwani yamekuwa hayana tija kwa wakulima kutokana na watumishi wa serikali kutoyapa kipaumbele.
Mbali na hilo wengine walisema licha ya serikali kujinadi kwa kutangaza kuwa Tanzania inakuwa kiuchumi bado watanzania wana hali mbaya na uenda utafiti uliofanywa umewahusisha watu wenye kipato kikubwa.
Kwa upande wake mmoja wa mjasiliamali kutoka katika halmashauri ya Chamwino ambaye anafanya biasharawa nyama na ngozi,Mosses Mdulanii,alisema kuwa kwa sasa hali ya uchumi imekuwa mbaya zaidi kwa wananchi wa hali ya chini jambo ambalo limesababisha wafanyabiashara wadogo kushindwa kufanya biashara.
“Awali tulikuwa kukifanya biashara ya kuuza nyama ya ngombe angalau tulikuwa tunachinja ng”ombe watatu kwa siku na tunamaliza lakini kwa sasa tunachinja ng’ombe mmoja na tunashindwa kumaliza nyama.
“Tunaishangaa serikali kudai kuwa uchumi umekuwa lakini kwa watu wa hali ya chini bado uchumi ni mgumu sana ni vyema serikali ikaruhusu upatikanaji wa fedha ili mzunguko uweze kuwa mkubwa na hapo itakuwa nafuu kwa wafanya biashara wa chini” alieleza Mdulanii.
Naye mjasiliamali ambaye anajihusisha na ufugaji wa nyuki kutoka Chiboli wilayani Chamwino, Bahati Thadei, alilalamikia maandalizi mabovu na kusema yamelazimisha maonesho ya Nane nane kudolola.
“Tumejikuta katika banda hili la Chamwino tukiwa wawili tu hatujui halmashauri inawaza nini kwa maana hakuna maandalizi yoyote yanayoendelea hapa tunajiuliza ni nini kitafanyika ebu, jiulize leo ni tarehe mbili lakini hakuna jambo lolote linaloendelea”alisema Thadei.
Hata hivyo kurugenzi wa Halmashauri ya Chamwino,Athumani Masasi, alitopatafutwa kwa njia ya simu ili aweze kuzungumzia swala hilo alijibu kuwa hayuko tauari kujibu maswali hayo wala kutoa majibu kwa sasa.
Baada ya muda mfupi alipiga simu ya mkonono huku akilalama na kutaka kujua ni kwanini anapigiwa simu kwa ajili ya kutoa maelezo ya nane nane hata kama banda la halmashauri lina watu wawili tu.
“Sasa nataka nikupe ushauri mimi sina taarifa zozote za maandalizi ya nane nane na hujuli nilipo na mbaya zaidi kwanini umetumia simu ya mtu mwingine na kwanini hukutumia simu yako sasa nakupa ushauri kama unataka kujua maandalizi ya nane nane njoo huku ofisi za halmashauri ili upatiwe mtu ambaye atakupa maelekezo”alisema kwa kufoka Mkurugenzi huyo
Kwa upande wa maandalizi kutoka katika halmashauri ya kongwa viongozi wa halmashauri hawakuweza kupatikana wala kueleza ni kwanini hawakuweza kufanya maandalizi ya nane nane licha ya kuwa yalitakiwa kufanyika kwa muda mrefu.
Naye mmoja wa washiriki katika maonesho ya Nane nane,kutoka halmashauri ya Singida,ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema ukata unaozikumba halmashauri nyingi mbalimbali hapa nchini umesababisha maadalizi ya nanenane kuzolota.
Alisema yeye amefika katika viwanja vya maonesho lakini hakuna maandalizi yoyote jambo ambalo kama siyo watumishi wa serikali kudharau maonesho hayo ni bora yasiendeleo kuoneshwa kwani kwa kufanya hivyo ni sawa na kutowatendea haki wananchi ambao ni wakulima.
Akitolea ufafanuzi wa kudolola kwa maonesho ya nane nane kanda ya kati katibu wa maonesho hayo kanda ya kati Aziza Mumba,alisema wataalamu wengi wa serikali hawana ubunifu.
Kuhusu mabanda yaliyoshindwa kufanya maandalizi kama vile banda la halmashauri ya Chamwino,Kongwa,Singida na Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi, alisema ni tatizo la kushindwa kujipanga katika kufanya maandalizi.
“Licha ya kuwepo kwa migogoro ya TASO lakini hilo haliwezi kuwa kisingizio,mbona halmashauri ya Kongwa imeweza kufanya vizuri na ina maandalizi mazuri, lakini nataka kusema kuwa wataalamu wengi wa halmashauri hawana ubunifu katika maeneo mbalimbali ya kazi.
“Kweli katika halmashauri za serikali za mitaa wanaotakiwa kushiriki kikamilifu hawakuweza kushiriki vizuri lakini najua nane nane ijayo maandalizi yatakuwa mazuri na tutakuwa na washiriki wengi wan je na wandani kwa maana ijulikane wazi kuwa kama hakuna kilimo bora haiwezekani kupatikana naTanzania ya Viwanda maana bila kuwa na wakulima wenye kuzaliza mazao bora utasindika nini katika viwanda hivyo” alisema Mratibu Mumba.