Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 9:37 am

NEWS: MAAMBUKIZI VIRUSI VYA CORONA MAREKANI YAFIKIA 215,000

Zaidi ya watu 5,000 wamefariki dunia nchini Marekani kwa sababu ya ugpnjwa wa Corona, ambapo zaidi ya watu 215,000 nchini humo wameambukizwa virusi hivyo, shirika la habari la AFP limeandika.

Donald Trump and the Coronavirus "Hoax" | National Review

Hii ni baada ya watu mia nane themanini na nne kuripotiwa kufariki dunia katika masaa 24, japo idadi hiyo ya Marekani ni ya chini ikilinganishwa na Italia na uhispania wakati huu maafa zaidi yakitrajiwa.

Rais wa nchi hiyo Donald Trump ametangaza kwamba anatathmini juu ya uwezekano wa kusitisha safari za ndege za ndani katika miji ya Marekani iliyoathiriwa zaidi na janga la Covid-19 (Corona), ambalo linaweza kuua watu wasiopungua 100,000 nchini humo, kulingana na ripoti ya mamlaka ya afya ya nchini Marekani.

National coronavirus updates: US surpasses 4,000 deaths as number ...

"Tunatatmini hili, lakini mara tu hatua kama hiyo itakapochukuliwa, tutakuwa tumefunga sekta ambayo ni muhimu sana," Rais wa Marekani amesema wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Ikulu ya White House.

Jumanne wiki hii Donald Trump alionya, siku mbili baada ya kuongeza hatua za kuangamiza janga la Corona hadi mwisho wa mwezi wa Aprili, kwamba wiki mbili "mbaya zaidi" zinatarajia kushuhudiwa nchini Marekani katika vita dhidi ya ugonjwa huo.

Rais wa Marekani alitangaza Machi 11 kwamba anapiga marufu raia wa nchi ishirini na sita za eneo la Schengen kutoka Ulaya kusafiri kwenda Marekani, kwa muda wa siku 30, ili kukabiliana dhidi ya kuenea kwa ugonjwa huo hatari.