Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 2:55 pm

NEWS: MAALIM SEIF ATAKA KUWEPO MJADALA WA KITAIFA JUU HALI YA KISIASA NCHINI

Zanziber: Katibu mkuu wa chama cha CUF Maalim Seif Sharifu Hamadi amesema kuwa anaona ipo haja ya kuwepo kwa mjadala wa kitaifa Juu ya hali Tete ya kisiasa nchini, akiandika kwenye ukurasa wake wa twitter, Saif anavitaka vyombo husika kuitisha haraka mjadala wa kitaifa ambao utazungumzia matukio yanayo tokea kwa sasa nchini " Serikali ya "Jamhuri ya Muungano inapaswa kuitisha haraka Mjadala wa Kitaifa juu ya Hali Tete ya Kisiasa iliopo ndani ya #Tanzania."

Seif ameonesha matukio manne ya hivi karibuni ambayo mpaka leo hayana majibu yake , lakwanza ni tukio la kutekwa kwa msanii Roma mkatoliki, kutishiwa bastola Mbunge wa mtama Nape moses Nauye mchana kweupe, kuchomwa moto kwa ofisi za mawakili wa IMMMA Advocates na tukio la hivi karibuni la shambulio lamkupigwa risasi la mbunge Tundu Lissu mjini Dodoma.


Seif amesema kuwa mamlaka za Uchunguzi nchini Tanzania yapo kisiasa sana na wanaonesha wamefeli kusimamia usalama wa Raia "The local investigative authorities are extremely politicized & have completely failed to restore confidence & reassure public safety."


Seif amejaribu kusema alichokisema mbunge wa kigoma ujiji Zitto kabwe kuwa kulingana na matukio yanayotokea nchini kukosa majibu kwa sababu ya kuwepo kwa watu wanaoitwa wasio julikana ipo haja ya kuwa na uchunguzi wa kimataifa, ambapo kwa upande wake seif amependekeza kabisa uchunguzi wa kimataifa ufanywe na FBI na scotland yard, "FBI & ScotlandYard should lead an independent international-led investigation into these murderous crimes committed by the "Unknowns".