Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 3:40 am

NEWS: MAALIM SEIF AMPA MANENO MAKALI MSAJI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI

SEHEM YA 1
Dar es salaam: Katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif sharif Hamad jana amemuandikia Barua yenye kurasa saba Msajili wa vyama vya kisiasa nchini Jaji Francis S.K.Mutungi, ikimtaka Msajili huyo kuheshimu Katibu ya CUF na Kujibu barua aliyomwandikia Jaji huyo juu ya kufukuzwa uwanachama wanachama saba wa CUF.


Seif alianza kwa kumuomba radhi Jaji Mutungi kwa kuchelewa kujibu barua yake kwa sababu ya kuwa njee ya nchi, Seif katika barua hiyo amemueleza jaji mutungi kuwa Lipumba si mwanachama wa chama hicho kwahiyo si mwenyekiti halali wa chama cha CUF kwa mujibu wa kikao cha baraza kuu la chama hicho.


". Hatimaye Mkutano Mkuu wa Taifa wa CUF ukaitishwa na Katibu Mkuu akatoa taarifa ya kupokea barua ya kujiuzulu kwa Profesa Ibrahim Lipumba nafasi yake ya Uenyekiti wa Taifa wa Chama. Nikaisoma barua yake mbele ya Mkutano Mkuu wa Taifa, na baada ya mjadala wa kina maamuzi yakachukuliwa kwa mujibu wa matakwa ya Katiba ya CUF ya 1992 (Toleo la 2014) kwa kupiga kura. Wajumbe 437 wakakubali kujizulu kwa Profesa Lipumba dhidi ya Wajumbe 14 waliokataa. Hivyo Profesa Ibrahim H. Lipumba kuanzia siku aliyojiuzulu si Mwenyekiti wa Taifa wa CUF. Profesa Lipumba hana mamlaka ya kukiongoza Chama chetu." alisema Maalim Seif katika barua hiyo.

Seif alimueleza Msajili kuwa baada ya Prof. Lipumba kumpelekea malalamiko Msajili juu ya kuvuliwa uwanachama alifanya maamuzi akiyaita ni msimamo wa ofisi ya msajili pasi kuonesha maamuzi hayo amepewa kwa mujibu wa sheria gani

"ningetarajia katika huo ulioita Msimamo ungeeleza kuwa kwa uwezo uliopewa na kifungu Na. kadhaa cha Sheria ya Vyama vya Siasa Na.5 ya 1992, au kwa mujibu wa uwezo uliopewa na Katiba ya CUF ya 1992 (Toleo la 2014) katika kifungu Na. kadhaa umeamua kumrudisha Profesa Ibrahim Lipumba kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa CUF. Lakini hukuweza kuonesha uwezo wako wa kisheria au kikatiba kumrudisha Profesa Lipumba kuwa Mwenyekiti wa Taifa CUF – Chama Cha Wananchi, kwa sababu huna uwezo huo kwa mujibu wa sheria za nchi wala kwa mujibu wa Katiba ya CUF."

Maalim amemshutumu Mutungi kwa kukivuruga chama Hicho bila kujali Kesi iliyofunguliwa mahakama kuu "Na tangu hapo umeendelea kuwa naye bega kwa bega katika kukivuruga chama chetu."


"Kesi inaendelea katika Mahakama Kuu. Kwa hali ya kawaida, ungetazamia kuwa wewe kama Msajili, na hasa ukiwa Jaji wa Mahakama Kuu hio hio usingeendelea kushirikiana na Profesa Lipumba kufanya vitendo ambavyo ni vya kihuni na vya hujuma dhidi ya Chama. Busara zingekuelekeza kumsihi Profesa Lipumba asubiri hukumu ya Mahakama Kuu, na kama angekataa wewe kama Msajili na Ofisi yako ungejitenga naye." aliandika seif kwenye barua hiyo.

Imeandikwa na Deyssa H.