Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 11:14 pm

NEWS: MAALIM SEIF AKABIDHIWA RASMI KADI YA UWANACHAMA ACT WAZALENDO

Dar es Salaam: Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, na Mbunge wa Kigoma Ujiji Zitto Kabwe amefanya tukio la Kihistoria baada ya kuwakabidhi kadi za uanachama wa chama hicho waliokuwa vigogo wa Chama cha Wananchi (CUF) huku Maalim Seif Sharif Hamad akipewa kadi namba moja na Juma Haji Duni akikabidhiwa kadi namba 10.

Shughuli ya kukabidhi kadi hizo inaendelea kufanyika leo Machi 19, 2019, makao makuu ya ACT- Wazalendo yaliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Viongozi wengine ambao wamekabidhiwa kazi ni Ismail Jussa, Mbalala Maharangande na Sheweji Mketo, Katika makabidhiano hayo, Zitto amesema hiyo namba kumi ambayo amekabidhiwa Duni ni kama mchezaji wa timu ya Liverpool Sadio Mane.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa kadi, Maalim Seif amesema yeye ni mara ya kwanza kukanyaga ofisi za ACT- Wazalendo lakini anajiona ni mwenyeji. “Nawashukuru sana kwa kukubali ombi letu kwamba tuje tuchangie nguvu katika chama cha ACT- Wazalendo na ninyi hamkuwa na ajizi mkatuambia njooni na haukuwa uamuzi wa viongozi pekee bali wa wanachama,” amesema Maalim Seif "Watu wameniuliza kuwa kwanini nimechagua Chama kidogo, lakini jibu ni kwamba hata wakati nafukuzwa CCM hakukuwa na chama kikubwa lakini hatukuacha siasa, tulianzisha CUF na ikawa na nguvu, hivyo ACTwazalendo ipo sehemu nzuri'

''Chama hiki kina kiongozi shupavu zitto kabwe mwenye maono, asiye na ubabaishaji na mwenye kufanya utafiti na akijiridhisha haogopi kutoa msimamo wake'' amesema Maalim Seif.