- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAALIM SEIF AENDESHA KIKAO KUMJADILI PROF. LIPUMBA
Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad ameitisha na kuendesha kikao cha dharura cha Kamati ya Utendaji ya Taifa ili kutafakari hatua ya Profesa Ibrahim Lipumba ya kuitisha mkutano mkuu wa taifa wa chama hicho.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 11 Machi 2019 na Naibu Mkurugenzi wa Habari, Mawasiliano na Umma, Mbarala Maharagande, kikao hicho kilianza kufanyika jana tarehe 10 Machi 2019 kuanzia saa 9.00 mchana na kumalizika saa 7 za usiku.
“Maalim Seif ameitisha kikao cha dharura cha kamati ya utendaji ya taifa kilichoanza saa 9 mchana 10/3/2019 na kumalizika saa 7 za usiku 11/3/2019 kutafakari hatua za kuchukua kutokana na kusudio la Lipumba na genge lake kutaka kukiuka, kupuuza na kuvunja kwa makusudi amri ya zuio ya Mahakama Kuu ya Tanzania iliyotolewa tarehe 28 Februari 2019.
“Zuio hilo lilitolewa na Mheshimiwa Jaji Stephen Magoiga kuzuia kuandaa na kuitisha mkutano mkuu wa taifa wa CUF mpaka pale shauri la msingi namba 84/2018 litakaposikilizwa na kufanyiwa maamuzi,” inaeleza sehemu ya taarifa ya Maharagande.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa, kamati hiyo imejadili mambo saba ikiwemo, taarifa ya Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara, Joran Bashange iliyoeleza kwamba, chama hicho kimepeleka nakala ya hukumu hiyo kwa vyombo vya dola.
“Ilijadili taarifa za kuwasili Dar es Salaam makundi ya watu kutoka sehemu mbalimbali wanaojipa hadhi ya kuwa wajumbe wa mkutano mkuu pasian kufanyika kwa uchaguzi wa ngazi za tawi, kata na wilaya kwa mujibu wa katiba ya CUF,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa, baada ya tafakuri ya kina kamati hiyo imetoa wito kwa wanachama wa CUF, viongozi wa chama, na wapenda demokrasia, kila mmoja kwa nafasi yake kushiriki kuhakikisha amri ya katazo la mahakama kuu linatekelezwa na mkutano wa Prof. Lipumba haufanyiki.