Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 4:58 am

NEWS: MAALIM SEIF ADAI CCM INAMPANGO WA KUIFUTA SEREKALI YA ZANZIBAR

Zanznbar: Katibu Mkuu wa Chama cha wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema wameigundua mpango wa chama cha mapinduzi CCM kutaka kuifuta serekali ya Zanzibar na kuifanya Tanzania yenye Serikali moja itakayoongoza Zanzibar na Tanzania bara yenye Rais Mmoja.

Maalim Seif aliyasema hayo Jumamosi ya wiki hii Feb 9 akizungumza na wanachama wa CUF katika ofisi ya Kilimahewa mjini Unguja.

Kwa upande wake katibu wa uenezi CCM Zanzibar, Catherine Peter Nao alikanusha madai hayo na akidai hiyo si ajenda ya chama chao na hawajawahi kufikiria suala hilo.

Maalim Seif alisema wanaamini mikakati inayoendelea kupangwa na kuratibiwa ikiwamo ya kununua wabunge inalenga kuifanya Tanzania kuwa na Serikali moja.

Akifafanua zaidi hata hivyo Maalim Seif alisema suala hilo haliwezi kukubalika kwa sababu Serikali ya Zanzibar ipo kwa mujibu wa katiba hivyo kuifuta ni kuivunja katiba.

Kuhusu migogoro iliyopo kwenye chama chao, alisema wanachama wamejiandaa na matokeo yoyote yatakayotolewa na Mahakama na kwamba, iwapo watashindwa haitakuwa mwisho wa harakati za kisiasa kwa upande wao. Naye Catherine alisema kila kitu kinaendeshwa kwa misingi ya kikatiba na ilani ya CCM, hivyo suala hilo halimo katika pande zote hizo.