- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MA DC WANAOWAWEKA WANANCHI NDANI HOVYO KUFANYIWA TATHIMINI
Dodoma: Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa (TAMISEMI) Seleman Jaffo amesema kwasasa wanafanya tathimini juu ya mwenendo wa Wakuu wa mioka na Wakuu wa wilaya wanaofanya vitendo vya kuwaweka wananchi na wawekezaji ndani hovyo.
Kauli hiyo Jaffo ametoa leo Jumanne April 9, 2019 mjini Dodoma mara baada ya Mbunge wa Rombo (Chadema) Joseph Selasin kumuuliza swali Waziri huyo juu ya vitendo vya baadhi ya wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa kutumia badaraka yao vibaya hasa kuwaweka ndani wawekezaji na wananchi licha ya serekali kukemea jambo hilo.
Selasin ametolea mfano Mkuu wa Wilaya ya hai na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi kuwa vinara wa kuwaweka ndani hovyo wawekezaji na wananchi mbalimbali pia na vitendo vya kutumia vikosi vya usalama kuwalazimisha baadhi ya wanasiasa kuhama vyama vyao.
Akijibu swali hilo Bungeni Dodoma Waziri Jaffo amekiri kuwepo kwa vitendo hivyo na wao kama Serekali kuu wemekuwa wakifanya tathimini juu ya vitendo hivyo " nikweli Mh. Mbunge unafahamu kwamba tulipotoka huko mwanzo hali ilikuwa mbaya sana, tulikuwa na idadi kubwa sana ya wakuu wa miko, wakuu wa wilaya na hali kadhalika wakurugenzi wa halimashauri lakini hasa hasa wakuu wa wilaya, walikuwa wakifanya mambo ya sivyo, lakini kazi kubwa inaendelea kufanyika" amesema Jaffo
"tunajua sisi ndani tunafanya tathimini hali imebadilika sana, lakini katika tabia za binaadamu kuna kesi by kesi na hata hayo mambo unayozungumza hivi sasa mengine yapo katika Utaratibu wa kuyashunghulikia kwa hiyo tuvute subra sio kila kitu kukitangaza hadharabi" amesema waziri Jaffo