- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: LUGOLA AWATAKA WAMILIKI VYOMBO VYA MOTO KUTOA MIKATABA YA KAZI
Morogoro: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kage Lugola amewataka wamiliki wote wa vyombo vya moto nchini kutoa mikataba ya kazi kwa madereva na wafanyakazi mbalimbali katika makampuni yao.
Waziri Lugola ametoa agizo hilo baada ya kuwatuliza madereva wa vyombo vya moto waliotaka kugoma kutokana na kutopewa mikataba ya kazi, matumizi mabaya ya tochi pamoja na ulipaji wa faini na kusimamishwa hovyo na matrafiki mabarabarani.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumapili Mei 19 katika Ukumbi wa Mikutano wa Bwalo la JKT Umwema, mjini Morogoro, Lugola pia ameonya madereva wanaopanga kufanya mgomo kuwa kufanya hivyo ni kukiuka sheria. Madereva hao walipanga kufanya mgomo kushinikiza mabosi wao kuwapa mikataba ya kaziAidha Waziri Lugola ameagiza Askari wanaopiga Tochi barabarani kudhibiti mwendokasi wapige Magari picha kwa mbele na sio nyuma na pia kibao cha spidi ni lazima kionekane kwenye hiyo picha, kama hakitoonekana basi Askari ndio atalipa faini na sio Dereva