- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: LUGOLA AWATAKA POLISI KUWAKAMATA WAPINZANI WANAOMTUKANA RAIS MAGUFULI
Morogoro: Waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi wa Tanzania Kangi Lugola amewataka Makamanda wote wa Polisi Nchini, kuwakamata wapinzani wote wanaomtukana Rais Dk. John Pombe Magufuli, kupitia vikao vyao vya siasa vya ndani ya chama.
Lugola ametoa kauli hiyo leo Jumapili Machi 10, 2019 wakati akizungumza na Wananchi wa Mji wa Kilosa, Mkoani Morogoro, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mjini humo, Pia Lugola amewataka Polisi kuwakamata watu ambao wanapora ardhi za wananchi wenye kipato cha chini, Wilayani humo.
Waziri Lugola amewahi kunukuliwa na Vyombo vya habari akiwaonya wananchi na viongozi wanao tumia mitandao yao ya kijamii vibaya ya kumtukana Rais Magufuli na kuwahidi wale wote watakao fanya hivyo dhidi ya Rais Huyo atakula nao sahani moja.
Lakini kwa mujibu wa sheria zetu za nchi kosa la kumtukana mtu yeyote, mtu huyo atakuwa ametenda kosa la jinai ambapo ni kinyume Cha sheria ya Kanuni ya adhabu , sura ya 15(89)1 ambapo hukumu yake ukipatikana na hatia ni kifungo cha miezi 6 jela