- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: LUGOLA AWATAKA POLISI KUTOWABAMBIKIA KESI WANANCHI
Arusha: Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amewataka polisi mkoani Arusha, kuacha tabia ya kuwabambikia kesi wananchi na badala yake wanapaswa kukamata wahalifu tu.
Kauli hiyo ya Lugola ameitoa katika mfululizo wa mikutano yake ya hadhara mkoani Arusha, katika wilaya za Arusha mjini, Arumeru na Monduli
Jana Ijumaa Februari 15, 2019, Lugola alisema wajibu wa polisi ni kulinda raia na mali zao hivyo ni wajibu wao kutimiza wajibu huo.
Lugola aliwataka polisi wa wilaya ya Arumeru, kuhakikisha wanakamata watuhumiwa wa ubakaji na wanaowapa mimba wanafunzi.
"Tunawataka watuhumiwa wote wa ubakaji kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya dola," alisema.
Lugola alitoa kauli hiyo, kutokana na malalamiko ya Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Amina Mollel kuhusiana na kutokamatwa kwa watuhumiwa wa ubakaji na waliowapa mimba wanafunzi.