- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: LUGOLA AWAONYA WANAOTAKA KUFANYA MIKUTANO YA HADHARA
Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, Kangi Lugola amevionya vyama vya siasa nchini ambavyo vimetangaza kufanya mikutano ya hadhara kabla ya muda uliopangwa kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa nchini.
Akizungumza leo Ijumaa Agosti 30, 2019 katika mahojiano maalum na chombo kimoja cha habari jijini Dar es Salaam, Waziri Lugola amesisitiza kuwa, Jeshi la Polisi lipo imara kipindi cha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019 pamoja na Uchaguzi Mkuu mwakani.
“Hii naomba nieleweke na pia iwekwe akilini, mikutano ya hadhara bado haijaruhusiwa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa, ni kosa kufanya mikutano ya hadhara kabla ya tarehe ya kufanya mikutano ya hadhara pamoja na kampeni haijatangazwa,” alisema Lugola.
“Jana kuna chama kimetangaza kuanza kufanya mkutano wa hadhara, sasa waendelee na mipango yao, halafu tuone nini kitawatokea. Nimekabidhiwa lindo hili na Rais (John) Magufuli ili niweze kulilinda ipasavyo, hivyo basi, wanasiasa wasubiri muda wa kuanza kampeni na sio kukurupuka kufanya mikutano ya hadhara bila ya kufuata taratibu, hilo halikubaliki hata kidogo,” alisema.
Waziri Lugola alionyesha kushangazwa kama kuna baadhi ya vituo hivyo kuendelea kuvunja maagizo yake ya kutoa dhamana saa 24. “Mwananchi yeyote atakayenyimwa dhamana au atakayeonewa, hakikisheni mnanipigia simu na pia kuna njia nyingi za kutupa hapa wizarani kupitia mitandao yetu ya kijamii, tovuti pamoja na makamanda mbalimbali walipo katika mikoa yote nchini,” alisema Lugola.