Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 10:51 am

NEWS: LUGOLA AMTAKA MKUU WA USALAMA BARABARANI KUJITASMINI KAMA ANATOSHA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amemtaka Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Fortunatus Musilimu, kujitafakari kutokana na rushwa iliyokithiri na uonevu kwa wenye magari Hapa nchini.

Akizungumza leo Jumatano Januari 16, 2019 na waandishi wa habari jijini Dodoma lugola amedai kwamba kumekuwa na utaratibu wa askari wa usalama barabarani kuwabambikizia watu kesi huku wakichukua rushwa wazi wazi bila kificho.

“Askari wa barabarani wamekuwa wakiwatoza watu kwa makosa ambayo hayaeleweki, namuomba Kamanda wa Usalama Barabarani ajitafakari,” amesema.

Katika hatua nyingine Waziri huyo wa Mambo ya Ndani ya Nchi amewasimamisha kazi makamanda watatu wa polisi kwa makosa mbalimbali ikiwemo kutotii maagizo yake.

Makamanda waliosimamishwa kazi ni pamoja na wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala Salum Hamduni, Temeke, Emanuel Lukula na wa Arusha Ramadhan Ng’azi.

“Sababu za kuwasimamisha Kamanda wa Ilala na Temeke ni kutotii maagizo yangu ya kusimamia rushwa kwa askari na yule wa Arusha kutokana na kushindwa kusimamia dawa za kulevya ikiwamo mirungi,” amesema Lugola.