Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 7:48 am

NEWS: LUGOLA AAGIZA KUKAMATWA WANAOSAMBAZA TAARIFA ZA KUTEKWA WATU

Waziri Kangi Lugola ameliagiza Jeshi la Polisi nchini, kuwakamata watu wote wanaosambaza taarifa za uongo, juu ya matukio ya utekaji au kupotea kwa watu, kwa kile alichokieleza baadhi yao wanalengo la kupata umaarufu wa kisiasa.

Waziri Lugola, ametoa kauli hiyo leo July 14, 2019 wakati akizungumza na Wananchi wa Kisorya, katika Jimbo la Mwibara,Wilayani Bunda.

kumekuwa na tabia ya watu kutekwa nyara nchini Tanzania hatua ambayo inatengeneza taswira ya uwoga dhidi ya nchi iliyokuwa imejizolea umaarufu kwenye sura ya dunia kuwa na amani na utulivyo tangu kupatikana kwa uhuru mwaka 1961.

Hivi karibuni mfanyabiashara wa Tanzania raia wa kenya Raphael Ongangi alitekwa Jumatatu usiku katika viunga vya mitaa ya Oysterbay jijini Dar es Salaam na watu wenye silaha akiwa na mke wake Veronica Kundya. na baadae julai 2, 2019 akapatikana jijini mombasa nchini Kenya.

Julai 7 mwaka huu Allan Kiluvya ambaye anatajwa kuwa ni msaidizi wa Waziri mstaafu wa Mambo ya Nje ya wa Serikali ya awamu nne, alidaiwa kutekwa na kupotea baada ya kuchukuliwa na watu wasiojulikana usiku.

Mwanaharakati wa chama cha upinzani nchini Mdude Nyagali alitekwa kwa siku tatu kabla ya kujipata porini katika eneo la Mbeya.

Mdude ambaye aliokolewa na wanakijiji ambao walimpeleka katika hospitali ya eneo hilo alipatikana akiwa mchovu na aliyeteswa wakati wa kipindi chote cha utekaji wake.

Sakata la matukio ya mauaji, utekaji na watu kupotea hapa nchini Tanzania limewahi kutua bungeni dodoma baada ya mbunge Peter Msigwa kuomba hoja ya dharura ili bunge liweze kujadili matukio hayo ambapo kulingana na mbunge huyo yamekuwa yakiendelea na hivi karibuni mtu mmoja aliyejulikana kwa jina Mduda Nyagali ametekwa na watu wasiojulikana huko wilayani Mbozi mkoani Songwe huku jeshi la polisi likilalamikiwa kutochukua hatua yoyote.

Akizungumza bungeni mjini Dodoma, Mbunge Peter Msigwa wa CHADEMA amesema kuwa matukio ya mauaji, utekaji na watu kupotea yamekuwa yakiendelea nchini humo na hivyo kuendelea kuzua hofu miongoni mwa Watanzania huku serikali kupitia mamlaka zake husika likiwemo jeshi la Polisi kushindwa kuyatolea taarifa matukio hayo yanayokwenda kinyume na haki za binadamu na hivyo kulitaka bunge lijadili kwa dharura suala hilo:

Lakini wizara ya mambo ya ndani ya nchi, kupitia naibu waziri wake Hamadi Yusufu Masauni, alisema kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vimekuwa vikifanya kazi ili kukabiliana na matendo hayo huku akikanusha kuwa sio kweli kwamba hakuna hatua zozote ambazo zimechukuliwa na serikali.

Naibu waziri huyo mwenye dhamana ya usalama wa raia na mali zao alikwenda umbali wa kuliamuru jeshi la polisi kumuhoji mbunge Peter Msigwa ili athibitishe kauli yake aliyoitoa bungeni.