- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: LOWASSA AILAANI SEREKALI BAADA YA KUVUNJA KONGAMANO LAKE
DAR ES SALAAM: Aliyekuwa Mgombea Urais mwaka juzi na Waziri mkuu mstaafu wa Tanzania Eduard Ngoyae Lowassa amelaani kile anacho kiita kama Uminyaji wa Demokrasia nchini Ulio fanywa na Serekali ya Mkoa wa Dar es salaam kwa kuchukua hatua ya kuvunja Kongamano la kidemokrasia ambalo lilikuwa linaleta Watanznia pamoja.
Akizungumza jana na vyombo vya habari jijini Dar es salaam Lowassa alianza kwa kusema kuwa “Naomba unisikilize vizuri kama kunajambo hukulielewa nivyema ukaniuliza nikafafanua vizuri” akiwaambia waandishi wa habari na kusema kuwa huwa naongea kwa kifupi kwahiyo nivyema ukaniuliza swali kama haukunielewa,
Lowassa alieleza Dhamira yake ya kuitisha kongamano hilo kwa kusema kuwa “Dhumuni la kongamano Lilikuwa ni kuwaleta watanzania pamoja, ni kuzungumzia Demokrasi” alisema kuwa wakati ule wa tume ya Nyalali ilielezea kuwa Tupingane bila kupigana, nakusema kuwa kila mtu anamaoni yake “huyu bwana anaweza kuwa na maoni yake nami na weza kuwa na maoni yangu hakuna dhambi”.
Pia Lowassa alizungumzia kitendo cha Rais John Pombe Magufuli cha kuwaambia wananchi wa Moshi kuwa nawasamehe, Lowassa alihoji “Unawasamehe kwa kutokukupigia kura? Watu milioni sita have said NO.. na wanahaki ya kusema NO”.
Lowassa alitoa onyo kwa Chama tawala (CCM) kwa kusema kuwa ipo siku watakuja kuondoka madarakani “lakini kubwa zaidi nawaomba wezangu tena wa CCM wajue kwamba ipo siku nchi hii itatawaliwa nawatu ambao si wao, haiwezekani kila siku ni CCM CCM miaka nenda miaka rudi lakini ipo siku wataondoka madarakani”. kuwaharasi wengine simply because is opposition is a wrong and bad na nikuminya Demokrasi” alisema Lowassa.
Pia Lowassa aligusia swala la Mafuriko dhidi ya mvua zinazo nyesha nchini kwa kusababisha njaa na kusema vitu vimekuwa na bei juu. Pia Lowassa alionyesha masikitiko yake dhidi ya Serekali kwa Hatua ya kuwafukuza wafanyakazi elfu tisa serekalini na kusema kuwa nawapongeza serekali kwa kazi nzuri dhidi ya watu kufoji vyeti lakini aliwaomba serekali kufikiria vizuri wanachi waliotumikia Serekali vizuri kwa muda mrefu na kuwataka wawafikirie hata kwenye mafao yao angalau.