Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 12:33 pm

NEWS: LORI LAIGONGA TRENI NA KUJERUHI ABIRIA 32

Dodoma: Watu 32 wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha lori lenye usajili namba T 860 APW na treni ya Abiria katika eneo la Hazina jijini Dodoma

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Protas Katambi amesema leo asubuhi Jumanne Juni 18, 2019 kuwa ajali hiyo imetokea jana saa 5.30 usiku na ametoa maagizo kadhaa ikiwemo kumsaka dereva wa lori ambaye inasemekana aliruka kutoka kwenye lori baada ya ajali hiyo.

katika ajali hiyo imesababisha mabehewa mawili kuacha njia baada ya lori hilo kugonga treni.

lakini Mafundi wa shirika la Reli Tanzania wamejitahidi kurekebisha njia ya treni hiyo katika eneo la ajali ili kuwezesha njia hiyo kupitika tena.

Katambi amesema tayari wametoa maagizo kwa uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuondoa mabehewa yaliyoanguka pamoja na kuwatafutia usafiri abiria hao. "Bahati nzuri na Kamanda wa Polisi (Mkoa wa Dodoma- Gilles Muroto alikuwa hapa kwenye eneo la tukio ) kwa hiyo tuliagiza abiria wapewe ulinzi wa mali zao," amesema Katambi.