- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: LISSU: ''SPIKA WA BUNGE AACHE UNAFIKI WA FUTARI''
DODOMA: MBUNGE wa Singida Mashariki , Tundu Lissu (Chadema) amesema amemtaka Spika wa Bunge, Job Ndugai kuacha maneno ya unafiki kwa kulalamika kwamba wabunge wa upinzani wamekuwa wakisusia futari na shughuli nyingine za kijamii zinazoandaliwa na viongozi wa CCM
Lissu alisema Ndugai ni mnafiki kwani haiwezekani akaonesha upendo wa kuwataka wabunge wa upinzani kushiriki katika futari ambayo inaandaliwa na viongozi wa CCM wakati amekuwa akionesha ubaguzi na manyanyaso ya waziwazi katika vikao vya bunge vinavyoendelea.
Lissu ametoa kauli hiyo kutokana na kauli ya spika ya hivi karibuni kudai kuwa anashangazwa na viongozi wa vyama vya upinzani kuwazuia wabunge wao kutoshiriki katika futari ya pamoja iliyoandaliwa na Waziri Mkuu Kass Majaliwa huku akisema na yeye meabdaa futari ambayo ni vyema wabunge wote wakashiriki.
Mda mfupi kabla ya kuhairisha bunge Ndugai aliwaambia wabunge kuwa yeye ameandaa futari kwa ajili ya wabunge wote hivyo anawakaribisha wabunge kuhudhuria katika futari hiyo.
“Ndugu zangu waheshimiwa wabunge naomba niseme jambo hili leo kama mnavyojua nimeaandalia futari ili tuweze kujumuika wote.
“Lakini kuna jambo moja linashangaza sana na tunakoelekea siyo pazuri kama ikifikia kuwa eti wapo baadhi ya viongozi wanawazuhia wabunge kushiriki katika kula futali.
“Juzi Waziri Mkuu aliandaa futari lakini wapo viongozi ambao waliwazuia wabunge wao kushiriki,inapofikia hatua ya kutoshirikiana katika masuala la kijamii inakuwa siyo nzuri sana, lakini pia ijulikane kuwa futari ni sehemu ya ibada,na ndivyo mwenyezi mungu anavyoelekeza kwa mwezi kama huu mtukufu tinashirikiana kwa kutoa kile ambacho unacho kushirikiana na watu wengine”alieleza Ndugai.
Akizungumzia suala hili Lissu alisema Ndugai aache unafiki na kueleza kuwa naneno yake ni ya unafiki kabisa kwani awezi kuonesha kuwachukia,kuwanyanyasa na kuwabagua ndani ya ukumbi wa bunge na kutaka ushirikiano kwa kula futari.
“Ndugai aache unafiki tena mameno hayo ni ya unafiki kabisa yeye amekuwa akitunyanyasa wazi wazi,akituonea waziwazi na kutubagua wazi wazi,leo hii anataka eti tushirikiane katika kula futari hatuwezi.
“Ndugai amebinafsisha shughuli kwa serikali maana kwa sasa kiti cha spika,yeye spika na wenyeviti wake wanafanya kazi za serikali badala ya kufanya shuguli za kibunge kwa maana hiyo hatuwezi kushirikiana kwa kula futali wakati kuna uonevu mkubwa nadani ya bunge.
“Bwana mwandishi wewe mwenyewe unaona bunge linavyoendeshwa upinzania wanapangiwa cha kusema tukiomba mwongozo tunanyimwa tunaonewa,tunadhalauliwa,
Lissu alipoulizwa ni nini kitakachofanyika kutokana na kuonekana kuwepo kwa matabaka sasa alisema wapinzania watapanga na kuona njia gani ambayo itatumika ili kuondokana na uonevu wa wazi wazi unaofanywa na kiti cha Spika.
Hata hivyo siku za karibuni Spika Ndugai na Naibu Spika Dk.Tulia Askson walikana na kueleza kuwa bunge linaendeshwa kwa misingi ya kanuni,sheria na taratibu za Bunge na si Vinginevyo.
Viongozi hao pia waliwataka wabunge wote kusoma kanuni za bunge ili waone kanuni hizo zinawasaidiaje kupata haki zao pale wanapoona kuwa wanaonewa.