Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 9:31 am

NEWS: LISSU NI VIGUMU WAFANYAKAZI KUDAI HAKI ZAO KWA KUFANYA MAANDAMANO KWA MUJIBU WA SHERIA ILI HAKI ITENDEKE NILAZIMA.

Dodoma: Shirikisho jipya la Vyama Huru vya Wafanyakazi (TAFFETU), limeadhimisha siku ya wafanyakazi duniani- kitaifa mkoani hapa nalimetakiwa kujipambanua kwa kutokumbatia watesi wa wafanyakazi

Katibu wa Chama cha Wafanyakazi migodini (NUMET), Nicodemus Kajungu, amesema maadhimisho hayo yamejumuisha wanachama wa vyama vinavyounda shirikisho hilo, kufuatia kubaguliwa na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA).

Kati ya vyama 33 vya wafanyakazi vilivyosajiliwa nchini, ni vyama 12 tu vinavyounda TUCTA huku 21 vilivyobaki, ingawa vimetimiza masharti, vimebaguliwa na kukataliwa na TUCTA kwa visingizio visivyokuwa namashiko.

Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo, Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika(TLS), Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, Tundu Lissu, amewaasa wanachama wa TAFFET kutolkuungana na vyama ambavyo ni swahiba na watesi wa wafanyakazi.


Asili ya Mei Mosi, kwa mujibu wa Lissu, ni mauaji ya wafanyakazi Saba waliouawa kutokana na kugoma wakidai haki zao nchini Marekani, Mwaka1889 kabla maadhimisho hayo hayajaanza rasmi Mwaka 1904.

Lengo kuu la siku hiyo, lilielezwa naye kuwa ilikuwa ni wafanyakazi kudai haki na maslahi yao kwa maandamano na kwamba inashangazwa kwasasa siku hiyo imegeuzwa siku ya serikali.

“Wenzetu huko Moshi wamemuarika Mtukufu rais, kumuomba; hivi unaweza kuomba haki? Duniani kote watu waliopata haki zao hawakupata kwakuomba, bali waliidai na kuipigania,” ameeleza Lissu


Ingawa ameeleza kuwa amezungumza kwa niaba yake binafsi siyo makundi ya jamii anayoongoza, Lissu, amesema TLS wameazimia kuanzia sasa,kushughulikia matatizo yote ya wafanyakazi wote nchini, yanayohusu haki na maslahi kisheria.

Amesema wafanyakazi nchini wananyonywa, kwamba wapo wanaojiita wafanyakazi lakini kwenye mishahara na au marupurupu yao, hawatozwi kodi. Amesema rais na majaji, mishahara na marupurupu yao kisheria haitoziwi kodi na kwamba hata wabunge, ni mishahara tu inayotozwa kodi lakini marupurupu mengine ambayo hufikia takriban shilingi milini 7 kwa mwezi, kwa kila mmoja, haitozwi kodi.

Lissu,
ameitaka TEFFET kuendelea kujiimarisha kwani pamoja na kuwa wachache, wanaweza kuwa na nguvu zitakazowezesha kukomboa wafanyakazi katika ukandamizwaji na unyonywaji wanaokabiliana nao.

Amesema vyama vinavyodhani kuwa vikubwa, hata wanachama wake hawavipendi kwasababu wanafahamu ni maswahiba wa watesi wao, akasemaikiwa kweli TEFFET Iipo kwa ajili ya haki, lihakikishe ninadai na kuipigania na siyo kujigeuza ombaomba kwa serikali.

Alibainisha kuwa ni vigumu sana wafanyakazi kudai haki zao kwa kufanya maandamano, kwa mujibu wa sheria na kwamba ili haki itendeke ni lazima maandamano yafanyike kinyume cha sheria ingawa hilo likifanyika, serikali haitawaacha salama.