- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: LISSU KUANZA ZIARA ULAYA NA MAREKANI KUIANIKA SEREKALI
Dar es Salaam: Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu anatarajiwa kuanza ziara yake ya kikazi katika nchi mbili barani Ulaya kuanzia Jumatatu ya wiki hii Januari 28, 2019.
Anatarajiwa kufanya vikao kadhaa na viongozi wa Serikali na jumuiya mbalimbali katika nchi hizo mbili , pia atapata fursa ya kutoa mihadhara ya kitaaluma na kufanya mahojiano na vyombo vya habari nchi Ujerumani.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Januari 26, 2019 na ofisa habari wa Chadema, Tumaini Makene inaeleza kuwa Mwanasheria huyo wa chadema atakuwa nchini Ujerumani kwa siku mbili, ambako atakutana na baadhi ya maofisa wa Serikali na wabunge wa Bunge la Ujerumani.
Baadaye Lissu ambaye bado yupo katika matibabu licha ya kuruhusiwa kutoka hospitalini baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30, Septemba 7 mwaka 2017 akiwa Dodoma na watu wasiojulikana, atazuru makao makuu ya Jumuiya ya Ulaya (EU) mjini Brussels, Ubelgiji. Katika ziara yake hiyo ya Ubelgiji atakutana na baadhi ya watendaji wa jumuiya hiyo, wabunge wa EU na wanadiplomasia wa mataifa mbalimbali wanaowakilisha nchi zao EU.
Baada ya Ubelgiji, Lissu ataelekea Washington DC, Marekani kwa siku 10 ambapo mbali ya kukutana na Watanzania wanaoishi nchini humo, hasa katika maeneo ya Washington, Houston, Texas na Alabama, atakutana pia na maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.
Wengine atakaokutana nao Marekani ni watendaji wa Shirika la Kimataifa la Misaada la Marekani (USAID) pamoja na kamati za mabunge yote mawili ya Marekani zinazohusika na uhusiano wa nje (Afrika).
Akiwa mjini Washington DC, Lissu atakutana na kufanya mahojiano na baadhi ya vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa. Mnadhimu huyo wa kambi rasmi ya upinzani bungeni atahitimisha ziara hiyo kwa kufanya mhadhara mkubwa wa umma katika Chuo Kikuu cha George Washington (GWU)