- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: LISSU: 'HATUGOMEI MAHAKAMA TUNAGOMA KUPINGA VITENDO VYA UGAIDI'
DAR ES SALAAM: Mbunge wa singida mashariki ambaye pia ni mwanasheria wa chama cha CHADEMA Tundu Lissu amefunguka na kusema hawagomei mahakama au serikali au jeshi la polisi wanagoma ili kupinga ugaidi na vitendo vilivyo kinyume na utawala wa sheria wanavyoendelea kufanyiwa na wanasheria.
Lissu ameyasema hayo kupitia Ukurasa wake wa instagram
‘’Ni vizuri ikaeleweka kuwa hatugomei mahakama au serikali au jeshi la polisi tunagoma kupinga ugaidi nna vitendo vilivyo kinyume na utawala wa sheria walivyofanyiwa wanasheria’’ amesema
‘’Hatugomi kuhudhuria mahakama kwa sababu ya kutoa somo kwa mtu yeyote au kumuadhibu yeyote tunafanya hivyo kupinga mabavu, ,ugaidi,na kushambuliwa kwa mawakili wenzetu kama kitendo cha mshikamano.’’ Amesema
‘’Ukimya utatuweka hatarini kupiga kelele kupitia nyenzo tulionazo kutatuma ujumbe kwamba shambulio kwa mwanasheria mmoja, haliwezi na halitaweza kuvumilika . litatuma ujumbe kuwa bila ulinzi wanasheria hawatafanya kazi yao na hivyo hakutakuwa na utawala washeria’’ amesema Lissu
Kauli ya Lissu imekuja baada ya siku chache ofisi ya wakili wake Fatuma Karume zilizopo upanga jijini Dar es salaam kuungua moto na chanzo cha moto huo kutokujulika .