- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: LISSU ATANGAZA KURUDI NCHINI SEPTEMBA 7 MWAKA HUU
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) na mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani Bungeni Tundu Lissu ametangaza kurudi nchini hapa tarehe saba mwezi wa tisa kwa maana hiyo atakuwa ametimiza miaka miwili tangu aliposhambuliwa mjini Dodoma.
Akizungumza kwa njia ya simu na kupitia mtandao wa chama chake Chadema mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe katika makao makuu ya Chadema Lisu amesema kuwa atarudi nchini Tanzania siku hiyo ili kuadhimisha kushambuliwa kwake.
''Nitatua tarehe saba mwezi septemba 2019 kwenye ardhi ya tanzania kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa nitakuwepo, alisema Tundu Lissu
Baada ya Tangazo hilolimeonekana kuwafurahisha sana wanachama wadao na wafuasi wa chama hicho waliokuwa katika makao makuu ya chama kijitonyma jijini Dar es salam.
Septemba 7, 2017 aliposhambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana akiwa eneo la makazi yake Area D, Dodoma. Mara baada ya kushambulia, mwanasiasa huyo alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na usiku wa siku hiyo alihamishiwa Hospitali ya Nairobi nchini Kenya alikopata matibabu hadi Januari 6, 2018 na kuhamishiwa Ubelgiji kuendelea na matibabu zaidi.
Kwa mujibu wa taarifa ya chama kikuu cha upinzani CHADEMA kwa vyombo vya habari, tukio hilo lilitokea wakati mbunge huyo wa Singida Mashariki alipokuwa nyumbani kwake.
Tundu Lisu ni miongoni mwa wanasiasa wa upinzani nchini Tanzania ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya Tanzania.
Ametangaza kwamba yuko tayari kuwania urais 2020 iwapo vyama vya upinzani vitamridhia kufanya hivyo.