Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 10:33 pm

NEWS: LISSU ALAANI KITENDO CHA POLISI KUWAKAMATA VIONGOZI WA CHADEMA

Dodoma: Mbuge wa Singida mashariki na Mwanasheria mkuu wa Chadema Tundu Lissu ameonesho kuchukizwa na kitendo cha Jeshi la polisi kuwakamata na kuwafungulia mashtaka viongozi wa chama kikuu cha upinzani Chadema, na kusema kuwa vitendo hivyo vinamuweka Rais Magufuli kwenye Historia mbaya katika nchi ya Tanzania

''Hili wimbi la kukamata viongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini kwetu na kuwashtaki mahakamani kwa tuhuma za kijinga linamuweka Rais katika ligi ya kipekee kabisa katika historia yote ya nchi yetu.'' kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram Lissu alisema kuwa vitendo hivi ni sawa ,na wakati wa kikoloni ambapo wakoloni walikuwa wanatumia mbinu hizi dhidi ya TANU

"Wakati wa harakati za kudai uhuru wa Tanganyika, dola la kikoloni lilitumia sana mbinu hii dhidi ya TANU na viongozi wake. .

Wengi walifungwa na kufanywa 'prison graduates.' Wengine, kama Mwalimu Nyerere, waliponea chupu chupu kwa kulipa faini.

Lakini kama ambavyo mapolisi na magereza ya kikoloni hayakuweza kuua wazo ambalo muda wake ulikuwa umefika, vivyo hivyo mapolisi na magereza ya Magufuli leo hayataweza kuua wazo ambalo muda wake umefika. .
alisema Lissu


Pia lissu alisema kuwa ipo tofauti kubwa kati ya wakoloni wa kipindi hizo na Rais Magufuli

Tofauti ya Magufuli na wakoloni ni muda tu. Miaka sitini imeshapita kati ya wachochezi wa TANU na wachochezi wa CHADEMA. .

Wale wanaotutesa leo, watatupigia saluti kesho, Wanaotuita wachochezi leo, watatuita mashujaa kesho. Wanaomshangilia Magufuli leo, hawatataka kuhusishwa nae kesho. .