- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: LISSU AKATA TIKETI RASMI YA NDEGE KUREJEA NCHINI TANZANIA
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki ambaye pia ndio mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, amesema maandalizi ya kurejea kwake nchini Tanzania yamekamilika kwa ziaidi ya asilimia 90% na mapaka tiketi ya ndege tayari ipo kwenye begi lake.
Akizungumza na gazeti mmoja la tanzania la Nipashe kwa njia ya simu juzi akiwa Ubelgiji, alisema atarejea nchini Septemba 7, mwaka huu, kama alivyoeleza awali. Mwanasheria huyo alisema ameshafanya maandalizi yote muhimu ikiwamo kukata tiketi ya ndege itakayomrejesha nchini siku hiyo.
"Uhakika wa nini? Unataka nikuonyeshe tiketi ya ndege? Ninayo tayari na mpango wa kurejea upo palepale kama nilivyosema, ukisikia vinginevyo, niulize," alisisitiza.
Lissu anayetajwa kuwa huenda akapewa nafasi ya kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwakani, pia alisema yuko mbioni kukamilisha taratibu za kufungua kesi kortini kumshtaki Spika Ndugai kwa kumvua ubunge. "Mpango wa kufungua kesi hiyo taratibu zinaendelea maana inahitaji umakini mkubwa," Lissu alisema.
Mchana wa Septemba 7, 2017, Lissu (51), alishambuliwa kwa kupigwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana wakati akijiandaa kushuka kwenye gari lake, nyumbani kwake Area D jijini Dodoma, akitokea bungeni kushiriki kikao cha chombo hicho cha kutunga sheria.
Baada ya shambulio hilo la kinyama, Lissu ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Upinzani Bungeni, alilazimika kupatiwa matibabu ya kibingwa yaliyoanzia Hospitali ya Rufani ya Dodoma na siku hiyo hiyo usiku alihamishiwa katika Hospitali ya Nairobi, Kenya.
Lissu alikaa siku 121 katika hospitali hiyo ya Kenya hadi Januari 6, mwaka jana, alipohamishiwa Ubelgiji ambako Desemba 31, alimaliza matibabu yake ya awali na kuanza ziara katika baadhi ya nchi za Ulaya na Amerika.
Januari 19, mwaka huu, Lissu alihojiwa katika kipindi cha Dira ya Dunia cha Idhaa ya Kiswahili ya BBC na kuonyesha nia ya kugombea urais mwakani kama wanachama na viongozi wenzake wa Chadema watampa ridhaa hiyo. Januari 21, mwaka huu, Lissu alihojiwa kwenye kipindi cha HardTalk cha BBC na mtangazaji maarufu Stephen Sackur, kipindi ambacho kilizua mjadala mkubwa kutokana na namna alivyojibu maswali. Februari 20, mwaka huu, Lissu alifanyiwa upasuaji wa 23 aliodai ni wa mwisho kwenye goti la mguu wa kulia katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven, Gasthuisberg, Ubelgiji na akasisitiza kuwa baada ya upasuaji huo atarejea Tanzania.