Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 7:38 pm

NEWS: LISSU ACHINDA TUZO YA USHUJAA

Dar es salaam: Rais wa TLS na wanasheria mkuu wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ametangazwa katika kongamano la kimataifa lililofanyika jijini Lagos, nchini Nigeria, kuwa ndiye mwanasiasa kiongozi katika kutetea matumizi mazuri ya raslimali za taifa lake,


Wajumbe waliokusanyika kujadili amani duniani, wamesema: “Lissu ni kielelezo kizuri cha kiongozi mwenye maadili na shujaa wa haki za binadaamu… mpenda haki na mwanasiasa mkweli anayestahiki kuombewa na wapenda amani hata kufikia kuwa rais katika nchi yake.”

Kwa ujasiri wake katika kukataa dhuluma na kuitumia vema fani ya sheria katika kusimamia raslimali za taifa lake, wanakongamano wamesema, “mamilioni ya vijana duniani kote wameanza kuomba kusoma fani ya sheria vyuoni baada ya mitandao ya kijamii zaidi ya 11,000 kuripoti habari zake kwa muda wa siku 11 mfululizo kuliko habari za rais yoyote duniani.”