- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: LHRC WALILIA MCHAKATO WA KATIBA MPYA
Arusha. kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu (LHRC), pamoja na Wajumbe wa kongamano la Katiba lililoandaliwa na kituo hicho wametaka serikali kurejesha mchakato wa kupatikana Katiba mpya ili kumuenzi Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ambaye alipigania demokrasia ya kweli barani Afrika.
Matakwa hayo wameyasema leo Jumapilia Oktoba 13, 2019 katika kongamano hilo lililofanyika jijini hapa, wanasheria, Wanasiasa, wanahabari na wadau wa masuala ya sheria na haki za binaadamu, wamesema katika kuadhimisha miaka 20 tangu kufariki kwake, suala la kupatikana Katiba mpya ni moja ya mambo ya msingi ya kumuenzi.
Mratibu wa Kituo cha sheria na haki za binaadamu mkoani Arusha, Hamis Mayombo amesema kuna umuhimu kwa Watanzania wa kada zote kuungana na kuona haja ya kuwa na Katiba mpya itakayokuza demokrasia na kuchochea maendeleo nchini.
"Bado katiba mpya ina hitajika, mchakato wake ulishaanza lakini haujamaliza ni muhimu wadau wengi wakashirikishwa,” amesema Mayombo.
Fredrick Pallangyo amesema Tanzania kwa sasa imebahatika kuwa na Rais mzuri, (John Magufili) ambaye anafanya kazi kubwa ya kusimamia ukuaji wa uchumi.
Hata hivyo amesema, ili mambo anayoyafanya yawe endelevu, ni muhimu kuunda katiba mpya ambayo itaendeleza anachokiamini.
"Nimekuwa nikijiuliza kwa mfumo wa sasa, siku Rais Magufuli atakapomaliza muda wake je haya mambo makubwa ambayo anafanya yataendelea kweli kwa katiba ya sasa na hapa ndiyo naona ni muhimu tupate katiba mpya,” amesema Pallangyo.
Amesema ili kuendeleza miradi mikubwa ya umeme, barabara, ndege na uwajibikaji serikalini, ni muhimu kupata katiba mpya itakayoweka mambo hayo kwa upana wake na kusimamiwa na kiongozi yeyote atakaye chaguliwa.
Mratibu wa kongamano hilo, Raymond Kanegere kutoka LHRC amesema Katiba ndiyo msingi wa sheria zote hivyo, kupatikana mpya kutasaidia kuboresha sheria nyingi zinazolalamikiwa na wananchi.
“Katiba ni jambo muhimu sana katika uongozi wa Taifa lolote, LHRC inaamini katika maadhimisho haya ya miaka 20 tangu kufariki dunia Rais wa kwanza hayati Julius Nyerere jambo kubwa la kumuenzi na kupata Katiba mpya,” amesema.
Kongamano hilo limewashirikisha wadau wa masuala ya sheria, wanahabari na wadau wa masuala ya haki za binaadamu kutoka mikoa ya kanda ya Kaskazini, Morogoro na Dar es Salaam.