Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 7:43 pm

NEWS: LHRC IMEKUJA NA REPOTI, YABAINI UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAM TANZANIA

Dar es salaam: Kituo cha haki za binadam Tanzania LHRC Imetoa repoti yake leo juu ya mwenendo wa haki za binadam nchini Tanzania, akiongea mbele ya waandishi wa habari Mkurugezi wa kituo hicho Bi. Hellen Kijobisimba Amesema katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Juni, watu kadhaa wameuawa kwa sababu mbalimbali, ikiwamo tuhuma za ushirikina na watu kujichukulia sheria mkononi.

"Watu 115 wameuawa wakituhumiwa ni washirikina, kati ya vifo hivyo 23 vimetokea mkoani Tabora ambao unaongoza, ukifuatiwa na Kigoma wenye vifo 23 na Kagera vifo 11," amesema Dk Kijo-Bisimba.

Amesema matukio ya wananchi kujichukulia sheria mkononi nayo yamerudi kwa kasi kwani taarifa za Polisi zinaonyesha kuwa watu 479 wameuawa na wananchi wenye hasira.

Mkoa wa Dar es salaam ndiyo unaongoza kwa matukio hayo kwa kuwa na vifo 117 , ukifuatiwa na Mbeya vifo 33, Mara 28 na Geita 26.

"Taarifa ya kipindi hiki inaonyesha ukiukwaji mkubwa wa haki za raia hususani haki ya kuishi, lakini pia ukiukwaji mkubwa wa haki za makundi maalum hasa wanawake na watoto," amesema