- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: LEMA ATIKISA BUNGE APINGA MUSWADA WA SHERIA.
DODOMA: Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) amechafua hali ya hewa bungeni akipinga muswada wa mabadiliko ya sheria ya maliasili, wakati akichangia hoja hiyo huku akiwatuhumu wabunge wa CCM kufanya mambo kwa ushabiki.
Lema amesema sheria zilizoligharimu taifa mpaka sasa, zilipitishwa kishabiki bungeni, kama ambavyo wabunge wanataka kufanya hivyo sasa hivyo kama ushabiki utaendelea, lazima sheria zitakazopitishwa zitakuwa ni zilezile.
Naye mheshimiwa George Simbachawene, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, asimame na kumkosoa Lema kwamba alikuwa akikiuka sheria katika uchangiaji wake lakini alipokaa, Lema alimpiga kijembe kwamba anataka kubadilishiwa wizara ndiyo maana anapinga hoja ya Lema.
Akataka utengwe muda wa kutosha kujadili muswada huo na si kupeleka bungeni kwa hati ya dharura. Mjadala mkali uliendelea ambapo Lema aliendelea kutoa hoja nzito akizielekeza upande wa wabunge wa CCM.