November 26, 2024, 11:32 am
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: LAILA ODINGA AGOMA KURUDI KWENYE UCHAGUZI WA MARUDIO
Nairobi: Kiongozi na mgombea wa upinzani nchini Kenya NASA Bw. Raila Odinga amesema Tume ya Uchaguzi nchini humo haikuwashirikisha wapinzani kabla ya kutangaza tarehe mpya ya Uchaguzi wa urais ambayo imepangwa kufanyika tarehe 17 mwezi Oktoba.
Laila Odinga akitoa tamko
Odinga ametoa onyo kwa kusema kuwa uchaguzi huo uliopangwa hautafanyika iwapo majadiliano ya kina ya kina hayatafanyika kati ya wahusika wote ili kutatua tofauti mambo yanayozua mvutano ndani ya Tume hiyo.Muungano wa Upinzani NASA
Pamoja na hilo, Odinga amesema upinzani upo tayari kushiriki katika Uchaguzi huo mpya na kukosoa madai ya chama cha Jubilee kuwa hawataki kushiriki kwenye Uchaguzi huo.Hatua hii imekuja baada ya Tume ya Uchaguzi kutangaza kuwa wagombea wawili Uhuru Kenyatta na Raila Odinga ndio watakaokuwa katika karatasi ya kupigia kura.Ekuru Aukot
Nae mgombea wa chama cha Third Way Alliance Ekuru Aukot aliyewania urais , amekwenda katika Mahakama ya Juu kuitaka Tume ya Uchaguzi kuwaruhusu wagombea wengine kushiriki.